WANANCHI GHANA WAANDAMANA KUPINGA USHIRIKIANO WA KIJESHI NA MAREKANI


 
Maelfu ya wananchi nchini Ghana wameandamana kupinga kuongezeka mashirikiano ya kijeshi baina ya serikali ya taifa hilo na serikali ya marekani. waliandamana kattika mji mkuu wa Accra.

waandamanaji hao waliandamana kwa lengo la kuonyesha upinzani wao dhidi ya ushirikiano huo kwa kupiga ngoma na vuvuzeela huku wakiwa wamekusanyika kwa amani. baadhi yao walikuwa wamebeba mabango ambayo yalikuwa yanalaani kitendo hicho kwamba kinapingana na uzalendo kwa nchi yao na kinahatarisha uhuru wao.

Jeshi la polisi wanakisia kwamba takribani waandamanaji 3,500walihudhuria maandamano hayo na hakuna fujo yoyote ambayo ilifanyika.Jeshi la polisi lilikuwepo ili kulinda usalama wa waaandamanaji hao. Waandamanaji hao wameandamana baada ya bunge la nchi hiyo kupitisha mkataba huo wa mashirikiano ambapo marekani itawekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 20  katika mafunzo na vifaa kwa jeshi la Ghana. katika mkataba huo jeshi la marekani litaruhusiwa kuweka vikose vyake katika ardhi ya nchi hiyo pamoja na kutumia anga ya nchi hiyo pamoja na kuingiza vifaa vya kijeshi ndani ya nchi hiyo bila ya kulipia ushuru.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment