SHAMBA LA GRACE MUGABE LAVAMIWA

Shamba la aliyekuwa mke wa rais wa zamani wa zimbabwe Bi Grace Mugabe limevamiwa na wachimbaji wadogo wa madini. shamba hilo ambalo lipo katika eneo la mazowe. Shamba hilo lilivamiwa mnamo mida ya saa 5 na nusu mchana kwa mujibu wa ripoti ya polisi.Tukio hilo lilitokea mnamo machi 29

watu walioshuhudia tukio hilo wanadai walishangaa kuona wavamizi hao wakianza kung'oa limao ambazo zilikuwa zimepandwa katika shamba hilo.yakadiriwa kwa mujibu wa shahidi aliyeshuhudia tukio hilo anasema kwamba yakadiriwa watu zaidi ya 400 walihusika na uvamizi wa shamba hilo ambao walikuwa wanalenga kutafuta dhahabu.

shamba hilo lilikabidhiwa rasmi kwa familia ya mugabe kwa hati namba 6045 ambayo ilisainiwa na serikali ya zimbabwe mnamo juni mwaka 2016. mpaka sasa wavamizi hao wamekataa kutoka kwenye shamba hilo na wanalishikilia kimabavu
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment