SENETA NIGERIA ASHIKILIWA NA WAPIGA KURA WAKE


 

Seneta mmoja katika nchi ya nigeria ameshikiliwa na wananchi wake. wananchi hao wamemzuia seneta huyo kutokana na baadhi ya madukuduku waliyokuwa nayo ambayo seneta huyo ameshindwa kuwajibu. watu hao waliandamana mpaka ofisini kwake wakidai kwamba wana malalamiko ya mda mrefu ambayo seneta huyo hajayatatua.

Seneta huyo anayefahamika kwa jina la Joshua Lidani ambaye anawakilisha jimbo la Gombe kusini alidhibitiwa na wananchi wake wakati alipokuwa ana ziara katika jimbo lake. wananchi hao walizuia barabara na kumdhibiti seneta huyo na kumchukua kumpeleka kumficha kwa mda.
 taarifa hii imetolewa na shirika la habari la premium times ambalo liliipata kutoka kwenye ukurasa wa facebook wa mwanaharakati wa mitandao ya kijamii anayefahamika kama Ibrahim Wala. alikamatwa katika kitongoji cha talasse ambapo mashuhuda wanadai kwamba sehemu kubwa ya manung'uniko ya wananchi hao ni kwamba seneta huyo hajawahi kutembelea eneo hjilo tokea achaguliwe kuwa seneta
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment