MAREKANI YAONDOA MSAMAHA WA KODI KWA RWANDA

 media

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuondoa hadhi ya msamaha wa kodi kwa nchi ya Rwanda siku chache tu baada ya nchi hiyo kuzuia kuagizwa kwa mitumba kutoka nchini Marekani.
Hata hivyo wawakilishi wa biashara wa Marekani wanasema kuwa nchi za Kenya, Tanzania na Uganda na zenyewe zitakabiliwa na hatua kama hizi baada ya mataifa hayo nayo kutangaza kuzuia uagizwaji wa mitumba.
Vikwazo hivi vya Marekani kwa Rwanda vinatarajiwa kuanza kutekelezwa ndani ya siku 60.
Nchi nyingi za Afrika zilikuwa zimetiliana saini na Marekani chini ya makubaliano ya AGOA ya ubadilishanaji wa bidhaa na huduma na baadhi kutotozwa kodi, lakini hivi karibu nchi za Aftika mashariki zilitangaza kusitisha uingizwaji wa mitumba kutoka Marekani.
Nchi za Afrika Mashariki mwaka 2016 zilidai kuwa zitasitisha uagizwaji wa nguo za mitumba na viatu ifikapo mwaka 2019 ili kulinda viwanda vyao vya ndani.
Hata hivyo mwezi Machi mwaka jana, shirikisho la viwanda nchini Marekani lililalamika kwa Serikali likidai kuwa zuio hili la nchi za Afrika Mashariki litaathiri viwanda vya marekani.
Shirikisho hilo limedai kuwa ajira zaidi ya laki 4 za raia wa Marekani ziko hatarini kutokana na tangazo hilo la nchi za Afrika.
Shirikisho hilo limedai pia kitendo cha nchi za Afrika Mashariki kinaenda kinyume na makubaliano ya mkataba wa AGOA unaolenga kuhamasiaha biashara na nchi za kusini mwa jangwa la Sahara kupitia soko huru la Marekani.

SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment