KONGAMANO LA BIASHARA ZA KIISLAMU LAFANYIKA DAR

Kongamano ambalo lenye lengo la kuwahamasisha watu kufanya biashara kwa mujibu ya sheria za kiislamu lafanyika jijini Dar es salaam. Kongamano hilo limefanyika mnamo jumamosi ya machi 30  katika ukumbi wa hoteli ya city garden uliopo kariakoo katika jiji la Dar es salaam. Kongamano hilo liliandaliwa na taasisi ya STARA TANZANIA ambayo ni taasisi yenye malengo ya kuwajengea uwezo vijana kuweza kuasisi miradi ya kibiashara.


Watoa mada wakuu katika kongamano hilo alikuwa ni Suleiman Abdallah ambaye anayetokea katika kampuni ya SPM consulting na Hamis Busazi anayetokea kampuni ya HUD HUD. Mada ya kwanza ilikuwa ni namna ya kujua biashara halali kwa mujibu wa uislamu nay a pili iligusia namna ya kutumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara. Kongamano hili lilifanikishwa kwa ushirikiano uliopatikana kutoka kwa ISLAMIC FOUNDATION, STARA TANZANIA na HALAL PROJECT AMBASSADORS.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na idadi ya watu zaidi ya 100 ambao wengi wao walikuwa ni vijana


SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment