COSTA RICA YAPATA RAIS MPYA


 media
Mgombea wa mrengo wa kati-kushoto, Carlos Alvarado, ameshinda duru ya pili ya uchauzi siku ya Jumapili nchini Costa Rica, nchi iliyogawanyika kuhusu ndoa ya watu wa jinsia moja na dini.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Costa Rica, Carlos Alvardo, waziri wa zamani wa Kazi, ambaye amepata 60.7% ya kura, amemshinda mpinzani wake, mchungaji Fabricio Alvarado, ambaye alipata 39.3% ya kura.
Mchungaji Fabricio Alvardo, mwenye umri wa miaka 43, anayepinga ndoa za watu wa jinsia moja, katika hotuba yake mbele ya wafuasi wake, amekubali kushindwa na alimpigia simu mpinzani wake kwa kumpongeza.
"Hatukushinda uchaguzi, lakini tunaweza kukubali matokeo haya kwa moyo mkunjufu," amesema, kabla ya "kumshukuru Mungu kwanza".
Wakati wa kutangazwa kwa matokeo, wafuasi wa Carlos Alvarado walikusanyika kwenye eneo la mji mkuu, huku wakipiga kelele kwa furaha.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment