MAMA KANUMBA AANIKA WAZI KWAMBA ANATAMANI KUMTEMBELEA LULU

Akizungumza na shirika la habari la MCL Digital leo Machi 14, 2018 Flora amesema yeye kama mzazi anaumizwa na hali anayopitia Lulu na anatamani kwenda kumuona ili kumpa moyo, ila ndugu wa mwigizaji huyo wanamuona kama ndiyo chanzo cha kufungwa. Amesema wanaomlaumu wanapaswa waelewe kwamba yeye alishasamehe kwani hata angefungwa miaka 100, haiwezi kumfanya Kanumba arudi.
Tangu Lulu kahukumiwa nimekuwa nikipokea lawama na watu kunitusi kuwa mimi ndiyo sababu, huku wakisahau kwamba mimi nilishasamehe kama binadamu na siyo niliyekuwa mlalamikaji katika kesi hiyo isipokuwa alishatakiwa na Serikali,” amesema Flora na kuongeza: “Lakini yote namuachia Mungu kwa kuwa naamini kufungwa kwa msichana huyo hakuwezi kunirudishia mtoto wangu.”
 Novemba 13, mwaka jana Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia mwigizaji mwenzake, Kanumba. Siku ya Kanumba Wakati mwaka huu, Kanumba akiwa anafikisha miaka sita tangu afariki dunia ghafla, wasanii waliopitia mikononi mwake wanatarajia kuibeba siku ya Kanumba ambayo huadhimishwa Aprili 7 kila mwaka. Akilizungumzia hilo,
 Flora amesema mwaka huu shughuli hiyo imebebwa na wasanii hao kupitia kikundi chao kinachoitwa Soweto. Ameeleza ratiba ya siku hiyo, ni watu kukusanyika nyumbani kwake Kimara Temboni kuanzia asubuhi na baadaye wataelekea katika kaburi lake lililopo Kinondoni kwa ajili ya kufanya ibada, kisha kurejea tena nyumbani kwa ajili ya chakula cha pamoja.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment