KAMPUNI YA ASASI YAWASAIDIA SARE MADEREVA BAJAJI

KAMPUNI  ya   Asas Group  imetoa msaada  wa sare  kwa madereva  bajaji  100 zenye  thamani ya   zaidi ya shilingi  milioni  moja  katika Manispaa ya  Iringa  mkoani Iringa .
Mkurugenzi  wa kampuni ya  Asas ,Ahmed  Abri  akizungumza jana  katika  hafla ya bank ya  Finca  ya  kukabidhi mkopo  wa  Bajaji 15  katika  viwanja  vya  Mwembetogwa  jana  alisema  kuwa  kampuni  ya Asas  imeamua  kuwasaidia  bajaji  hao  sare  kama  ambavyo walivyoeleza  moja kati  ya  changamoto zao .
Alisema  kuwa  msaada  huo  wa  Sare  kwa  madereva  hao  utawawezesha  kuifanya kazi  hiyo katika  ufanisi na kuzingatia usafi  pindi  watoapo  huduma   hiyo ya  usafiri .
  Kuna  suala  moja  limezungumzwa na  afisa  biashara  wa Halmashauri na  Manispaa ya  Iringa  pia  mmelisoma katika  risala  yenu  juu ya  changamoto ya  sare  hivyo  sisi kama  kampuni ya  Asas   tumetafakari  na  kuamua  kujitolea   sare 100  kwa  ajili ya  kuanzia “
Hata   hivyo  aliwataka  madereva  hao   wa bajaji  kuwa  mfano kwa  kuheshimu  sheria  za  usalama barabarani   kwani  iwapo  wataheshimu  sheria  na  kujiepusha na  uvunjifu  wa sheria  kupitia kazi hiyo  wanaweza kupiga hatua   kiuchumi .
Pamoja na  kusaidia  sare  hizo  pia  alisema kampuni yake kwa  kutambua mchango wa bajaji  hao   na  kuwafanya  wajenge  utamaduni  wa  kunywa  maziwa  badala ya  pombe  pindi  wawapo  kazini  imeam ua  kuwapa  maziwa  ya  bure  madereva  wote  bajaji  300 na  wananchi  waliofika katika  hafla  hiyo  

Mwenyekiti  wa  Bajaji  mjini Iringa Norbert  Sunka  mbali ya  kupongeza  msaada  huo wa sare  alisema   kuwa kampuni  hiyo ya  Asas  imekuwa  msaada  mkubwa  kwa  madereva Bajaji  na kuwa  kupitia msaada  huo  wanaamini  madereva  wataifanya kazi hiyo  kwa kuzingatia  usafi wakati  wote .
Pia  mwenyekiti huyo  alisema kupitia  hafla  hiyo  meza  kuu akiwemo  mkuu  wa  wilaya ya mkurugenzi  wa kampuni ya  Asas  wameweza  kumchangia  pesa  ya  kununua Bajaji  mwanachamaa  wao  mwanamke  pekee  anayefanya kazi ya udereva bajaji kupitia  chama  hicho cha  bajaji .
Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  ambae  alikuwa  mgeni  rasmi katika hafla  hiyo   alisema  kuwa   hatua ya  kampuni  hiyo ya  Asas  kusaidia  sare  ni ukombozi  mkubwa kwa  madereva hao na  kuwa ni  mwanzo wa madereva  kuzingatia  usafi .
Aidha  aliwataka  madereva  bajaji na  vijana  wengine  wanaofanya kazi ya  kuendesha  boda  boda  kuepuka  kuhatarisha  afya  zao kwa  kunywa  ulanzi wawapo kazini na  badala yake   kujenga utamaduni  wa   kunywa  maziwa  kwa  afya  zao
 
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment