Wana wa ufalme wakamatwa Saudi Arabia


Saudi Crown Prince Mohammed bin Salman attends a conference in Riyadh, on October 24, 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionPrince Mohammed bin Salman
Mawaziri 11 miongoni mwao wakikwa wana wa ufalme wameachishwa kazi na hata kuzuiliwa katika Mabadiliko makubwa yaliyotangazwa kwenye serikali ya Saudia.
Wengine wanaozuiliwa ni mawaziri wa zamani ambao wamehusishwa na kashfa za rushwa.
Mwengine aliyekematwa ni billionaire Prince Al-Waleed bin Talal.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMwengine aliyekematwa ni billionaire Prince Al-Waleed bin Talal.
Katika hatua hiyo ambayo si ya kawaida inaelekea mwana mrithi wa mfalme Mohammed Bin Salman ambaye ndiye anaesimamia kitengo cha kupambana na ufisadi, anapania kujitenga na kuwadhibiti wapinzani wake wenye mamlaka makubwa nchini humo.
Miongoni mwa wanazuiliwa ni wana wa wafalme mmojawao ni mtoto wa marehemu mfalme Abdullah Prince Miteb aliyekuwa mkuu wa kitengo cha kikosi cha kiusalama National guard ambapo sasa amepokonywa wadhfa huo.
Saudi Arabian Prince Miteb bin Abdullah at the Elysee Palace in Paris, 18 June 2014Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPrince Miteb bin Abdullah ameondolewa kutoka kijiji chenye nguvu cha ulinzi
Mwengine ni billionaire Prince Al-Waleed bin Talal.
Inaripotiwa kwamba hisa katika kampuni aliyoekeza huko uingereza iitwayo Kingdom Holding, zimeporomoka kutokana na hisia hizo.
Mwandishi wa BBC anaefuatilia kwa karibu swala hilo anasema mabadiliko hayo bila shaka yatawabugudhi wale wanaopendelea mambo yabaki yalivyo Saudia ambako wenye mamlaka ya juu ya kiukoo na kikabila hawapendelei hatua kama hizo za kubadili mambo gafla.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment