Rais wa Ufaransa ziarani Saudi Arabia


Rais wa UfaransaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionRais wa Ufaransa
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye yuko nchini Saudi Arabia katika ziara isiyopanga, amesema atasisitizia umuhimu wa utulivu nchini Lebanon, katika mazungumzo yake na na viongozi wa nchi hiyo.
Ufaransa ina uhusiano wa karibu na Lebanon, na ziara hiyo ya Rais Macron imekuja siku moja baada Waziri mkuu Saad Hariri, kujiuzulu wakati alipokuwa Riyadh, hali inayochochea hisia kwamba alishinikizwa na Saud Arabia.
Awali akizungumza mjini Dubai, Rais Macron amesema anataka viongozi wa Lebanon kuishi huru ndani ya nchi yao.
Amesema pia atautaka uongozi wa Saud Arabia kusaidia kuzuia baa la njaa nchini Yemen, ambako muungano wa majeshi yanayoongozwa na nchi hiyo yamefunga bandari kuzia silaha kuingizwa nchini humo na kuwafikia wapiganaji wa Ki Houthi
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment