MKUU WA MKOA RUKWA AKATAZA KUUZA MAHINDI ZAMBIA

MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amewapiga marufuku wafanyabiashara wanaoingiza mahindi kwa magendo kutoka Zambia na kuyauza kwa bei ya kutupa akitaka waache mara moja.
Mheshimiwa Wangabo alisema mahindi hayo yanayoingizwa kwa magendo mkoani Rukwa kutoka Zambia ndiyo yamesababisha kurundikana kwa mahindi lakini pia kuendelea kuanguka kwa bei ya mahindi yaliyovunwa na wakulima mkoani humo katika msimu huu wa kilimo na hivyo kuathiri soko lao.
                   Aidha katazo hilo alilitoa wakati akijibu kilio cha wazee mkoani humo waliomweleza mahindi yamerundikana katika kila nyumba ya wakulima na wameshindwa kununua pembejeo za kilimo katika msimu huu. 
“.............Kila nyumba imefurika mahindi, hakuna pa kuyapeleka kwa sababu ya kutokuwepo kwa soko la uhakika na la ushindani .... Basi tumebakia kula asubuhi, mchana na jioni hata zaidi ya mara nne ....wasiwasi tutashindwa kununua pembejeo za kilimo kwani fedha hatuna kila mtu analia tu ...pia kuna hatari wakulima wakashindwa kulima msimu huu,” Mzee Joseph Ngua alimweleza mkuu wa mkoa
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment