Mahakama yamhukumu 'Lulu' miaka 2 jela kwa kifo cha Kanumba


Muigizaji Elizabeth Michale, maarufu kama 'Lulu
Image captionMuigizaji Elizabeth Michale, maarufu kama 'Lulu
Mahakama kuu ya Dar es salaam imemhukumu muigizaji wa filamu, Elizabeth Michale, maarufu kama 'Lulu', kifungo cha miaka miwili baada ya kumtia hatiani kwa kuua bila kukusudia msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.
Marehemu Steven Kanumba alifariki majira ya saa nane usiku,mnamo mwaka 2012 baada ya kutokea mzozo kati yake yake na Elizabeth Michael ambaye inaaminika kuwa walikuwa na uhusiano wa Kimapenzi.
Mahakama yamhukumu 'Lulu' miak 2 kwa kifo cha Kanumba
Image captionMahakama yamhukumu 'Lulu' miak 2 kwa kifo cha Kanumba
Kanumba, ambaye alijizolea umaarufu mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na hadi Afrika Magharibi baada ya kuwashirikisha katika filamu zake baadhi ya wasanii maarufu wa kutoka Nigeria akiwemo Mercy Johnson na Noah Ramsey.
Wasanii waomba usaidizi wa kumtafuta Roma Mkatoliki
Marehemu ambaye alizaliwa mwaka 1984, alianza kujipatia umaarufu mwanzoni mwa mwaka 2000 wakati huo akiigiza katika michezo ya runinga kupitia kundi la maigizo la Kaole Sanaa.
Mahakama yamhukumu 'Lulu' miaka 2 jela kwa kifo cha Kanumba
Image captionMahakama yamhukumu 'Lulu' miaka 2 jela kwa kifo cha Kanumba
Aliendelea na kuigiza filamu nyingi ambazo zilimpatia umaarufu mkubwa kiasi cha kusafiri mara kadhaa nchi za nje, ambako alitambulika kama mmoja wa wasanii wenye vipaji vikubwa ambaye aliitangaza fani ya filamu nchini Tanzania maarufu kama 'Bongo Movies.'
Mazishi yake yalichukua sura ya kitaifa kutokana na umaarufu aliojijengea msanii huyo katika jamii ya watanzania na hata nchi za nje.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment