JUKWAA LA AFYA LA DICOTA LAFANA, GREENBELT, MARYLANDMeza kuu kutoka kushoto ni Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Mhe. Wilson Masilingi, Naibu Waziri wa afya Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman,Mkuu wa kitengo cha Diaspora Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano Afrika Mashariki, Balozi Anisa  Mbega, Bi.Adila Hilal Vuai mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa wazanzibari wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) !, Bwn. Assenga kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Dr. Ali Salum Ali Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar. wakifuatilia jukwaa la afya lililoandaliwa na DICOTA katika kuwakutanisha wadau wote nje na ndani ya Marekani sekta ya afya kuwatambua na kuthamini mchango mkubwa wanaotoa katika sekta hiyo nchini Tanzania. Jukwaa la afya lilifanyika siku ya Jumamosi Novemba 11, 2017 Martins Crosswind Greenbelt, Maryland nchini Marekani. Picha naVijimambo Blog na Kwanza Production
Bwn. Lunda Asmani akiwakaribisha wadau wote na kufungua jukwaa la afya.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico akisoma hotuba yake kwenye kongamano la Afya lililofanyika siku ya Jumamosi Nov 11, 2017 Greenbelt, Maryaland nchini Marekani. Katika hotuba hiyo aliwashukuru DICOTA kwa kuandaa jukwaa hilo la wadau wa afya kwa kuthamini kazi kubwa inayofanywa na wadau hao na jitihada binafsi zinazofanywa kwa kusaidia ndungu zao nyumbani Tanzania pia alisema Rais Dkt John Pombe Magufuli anatambua na kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na Diaspora kwa nchi yao.
Balozi wa African Union nchini Marekani, Mhe.Arikana Chihombori Quao akichangia kwenye jukwaa hilo na kueleza changamoto nyingi nchi za Afrika inazopata katika sekta hiyo kutokana na miundo mbinu kuwa duni na sababu kubwa inachangiwa na wakoloni walivyoligawa bara la Afrika na kuwa nchi mbalimbali kwa kuogopa nguvu ya Afrika na utajiri wake usije ukaongoza Dunia.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman akiwashukuru Diaspora kwa mchango mkubwa kwa sekta ya afya Zanzibar na baadae kutoa salamu za Rais wa Zanzibar Mhe. Dr Ali Mohamed Shein kwa kutoa shukurani zake na kuthamini mchango mkubwa wa Diaspora hasa katika sekta ya Afya.
Balozi Anisa Mbega mkuu wa idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akishiriki jukwaa la Afya kwa kuwapongeza DICOTA kwa kuandaa jukwaa hilo na kuwakutanisha wadau wa afya na Serikali inathamini na kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Diaspora.
Balozi Liberata Mulamula akitoa shukurani zake kwa DICOTA kwa kuandaa jukwaa la afya na baadae kutoa mfano wa mtu akiwekewa fedha na afya bora yeye atakimbilia kwenye fedha kwa sababu hatambui umuhimu wa afya njema ni zaidi ya fedha kwa maana kwamba binadamu wengi hawaelewi umuhimu wa afya lazima tutambue hilo huku akitolea mfano mwingine wa nyani unapo mwekea fedha na ndizi yeye atachangau ndizi kwa sababu anajua bila ndizi maisha yake yapo hatarini. 
Dr. Mary Banda kutoka Jambo Tanzania akielezea jinsi alivyotumia elimu yake kwa kuelekeza nguvu yake kusaidia sekta ya afya mkoa wa Kagera.

Bi. Christine Lasway kutoka MyAfyaPal akielezea umuhimu wa afya na jinsi anavyoelekeza nguvu zake katika kusaidia sekta ya afya nchini Tanzania.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi


Bi.Tausi Suedi kutoka Childbirth Survival Tanzania akielezea jinsi alivyojikita katika kusaidia kuokoa maisha ya mtoto hasa wakati wa uzazi Tanzania kwa kutoa elimu kwa wakunga na wazazi kabla na baada ya kujifungua ikiwemo kwapelekea mahitaji muhimu kabla ya kujifungua.
Dr. Secelela Malecela kutoka Janet Weir Children's Hospital akieleza anavyoguswa katika kuelekeza nguvu zake katika sekta hiyo Dodoma.

Bi. Adila Hilal Vuai mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa wazanzibari wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) akitoa shukurani kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa jitihada za Diaspora katika sekta ya afya Zanzibar na kuwapongeza DICOTA kwa kuandaa jukwaa la Afya na kuwaasa kutumia lugha ya Kiswahili katika kuendeleza na kuthamini utamaduni wetu.

Dr. Frank Mimja akielezea umuhimu wa kusaidia sekta ya afya Tanzania na jitihada anazofanya kwa kupeleka madaktari Tanzania na kuwaelekeza wadau waliohudhuria jukwaa la Afya njia iliyosahihi kupitia katika kutimiza ndoto na azma yako ya kusaidia ndugu zetu Tanzania.

Kutoka kushoto ni Bwn. Lunda Asmani DICOTA, Bi. Adila Hilal Vuai kutoka Ofisi ya Rais Zanzibar na Dr. Ali Salum Ali Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.

Juu na chini ni wadau wa jukwaa la afya wakifuatilia jukwaa hilo wakati likiendelea.
Picha juu na chini ni wadau wa afya wakizungumzia na kubadilishana mawazo katika kuweka nguvu ya pamoja katika kusaidia sekta ya afya Tanzania.
Juu na chini ni picha za pamoja na wageni waheshimiwa,
Juu na chini ni mazungumuzo na wageni waheshimiwa.

Mahojiano yaliyofanywa na kwanza Production.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment