Tanzania yawatimua mawakili 3 wa Afrika Kusini waliohusishwa na itikadi za mapenzi ya jinsia moja


Rais John Pombe Magufuli
Image captionRais John Pombe Magufuli
Tanzania imewafurusha mawakili watatu wa Afrika Kusini waliokamatwa wiki hii wakituhumiwa kwa kukuza mapenzi ya jinsia moja.
Walikuwa miongoni mwa watu 13 waliokamatwa katika hoteli moja mjini Dar es Salaam .
Waandalizi wa mkutano huo wanasema kwamba mkutano huo ulikuwa umeitishwa kujadili iwapo wakabiliane na uamuzi wa serikali ya Tanzania kuzuia utoaji wa baadhi ya huduma za afya.
Mapema mwaka huu, serikali ilipiga marufuku baadhi ya kliniki za kibinafsi kutotoa huduma za ugonjwa wa HIV na ukimwi ikisema zilikuwa zikukuza mapenzi ya jinsia moja ambayo ni haramu nchini Tanzania.
Hatahivyo, Sibongile Ndashe anasema kuwa walikuwa hawana haki ya kuwakamata na ameishtumu mamlaka ya Dar es Salaam kwa kuwakamata yeye na wenzake.
Mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Tanzania.
Lazaro Mambosasa , afisa mkuu wa polisi mjini Dar es Salaam aliwaambia maripota kabla ya mawakili hao kukamatwa kwamba walikuwa wakikuza mapenzi ya jinsia moja.
Kukamatwa kwao kunajiri kufuatia hotuba ya mwezi Septemba iliotolewa na naibu waziri wa afya Hamis Kingwangala ambaye aliapa mbele ya bunge kukabiliana na makundi yoyote yanayounga mkono wapenzi wa jinsia moja nchini humo, kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Lakini bi Ndashe aliambia wanahabari hakuna makosa ambayo wangeshtakiwa nayo kwa kuwa mkutano huo haukuwa wa wapenzi wa jinsia moja .
Shirika la haki za kibinaadamu la Human Rights Watch limesema kuwa kundi hilo linaweza kuishtaki serikali ya Tanzania kwa kupiga marufuku vituo vya afya vinavyowauguza wato waliopo katika hatari ya kuambukizwa ukimwi mbali na uagizaji wa kifaa cha mafuta ambayo yanaweza kutumika kujilinda dhidi ya HIV.
Bi Ndashe anasema kuwa hatua yao ya kutaka kujua sababu za wao kutimuliwa nchini humo hazikuangaziwa.
Kundi hilo sasa limeonya kwenda mahakamani.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment