MKUFUNZI WA VETA AMEGUNDUA KIFAA AMBACHO KITAMLAZIMISHA DEREVA PIKIPIKI KUVAA KOFIA NGUMU

Tatizo la ajali za pikipiki linakaribia kupatiwa ufumbuzi wa kisayansi nchini tanzania. hiyo ni baada ya mkufunzi wa masuala ya ufundi katika chuo cha VETA Kipawa, AnethMganga, amebuni mfumo wa kielektroniki unaozuia pikipiki kuwaka mpaka dereva awe amevaa kofia ngumu (helmet). 

licha ya kusaidia katika kupunguza ajali kofia hiyo pia itasaidia  katika masuala ya usalama barabarani inasaidia kuzuia wizi wa pikipiki kwani mwizi hatoweza kuiwasha bila kofiangumu ambayo imeunganishwa kieletroniki. 

aidha kiu ya mtafiti huyo haijaishia hapo kwani bado anaendelea kufanya utafiti nakuboresha zaidi ubunifu huo, lakini ameomba serikali na wadau mbalimbali kuunga mkono ili uweze kuenea, kukubalikana kutumika na waendesha pikipiki katika maeneo mbalimbali nchini.

Mwalimu wa Elektroniki wa Veta Kipawa, Aneth Mganga akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda la VETA Pikipiki katika mojawapo ya maonyesho yaliyofanyika ndani ya mwaka huu

SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment