Marekani: Vitisho vya kinyuklia vya Korea Kaskazini vimeongezeka


Marekani inasema kuwa vitisho vya shambulio la kinyuklia dhidi ya Marekani vimeongezekaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionMarekani inasema kuwa vitisho vya shambulio la kinyuklia dhidi ya Marekani vimeongezeka
Tishio la shambulio la kinyuklia kutoka kwa Korea Kaskazini linaongezeka, amesema waziri wa ulinzi James Mattis wakati wa ziara yake nchini Korea Kusini.
Bwana Mattis ameonya kwamba taifa hilo litakabiliwa kijeshi iwapo litatumia silaha za kinyuklia.
Wakati huohuo Korea Kaskazini ililiwachilia boti moja la Korea Kusini ambalo ilisema lilipatikana limeingia katika maji ya Korea Kaskazini kinyume na sheria.
Wafanyikazi 10 wa boti hiyo waliachiliwa siku ya Ijumaa jioni , kulingana na maafisa wa Korea Kusini.
Hatua hiyo inajiri wakati ambapo kuna wasiwasi mkubwa katika eneo hilo, huku pande zote mbili zikifanya mazoezi ya kijeshi.
Korea Kaskazini imeongeza vitisho dhidi ya majirani zake na dunia nzima kupitia mpango wake wa utengenezaji wa silaha za kinyuklia, alisema bwana Mattis kulingana na AP.
Anasema kuwa Korea Kaskazini ilifanya tabia mbaya na kusema kuwa usalama wa Marekani na Korea Kusini umechukua hatua nyengine za dharura.
Waziri wa ulinzi wa Marekani James MattisHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionWaziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis
Washington haiwezi kukubali Korea Kaskazini inayoendelea na mipango ya kinyuklia, aliongezea, akizungumza pamoja na mwenzake wa Korea Kusini Son Young-moo.
Bwana Mattis yuko mjini Seoul kwa mazungumzo ya kila mwaka ya kijeshi na Korea Kusini.
Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kutembelea Korea Kusini mnamo mwezi Novemba katika ziara ya bara Asia.
Mapema mwezi huu, Marekani na Korea Kusini pia walifanya zoezi la kijeshi katika maji yanayozunguka rasi ya Korea wakishirikisha ndege za kijeshi, silaha na meli za kubeba ndege.
Zoezi hilo liliikasirisha Korea Kaskazini na Pyongyang na imekuwa ikisema kuwa ni zoezi la kujiandaa kwa vita.
Vilevile, Marekani imewaekea vikwazo raia saba wa Korea Kaskazini na kampuni tatu kutokana na unyanyasaji wa haki za kibinaadamu.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment