LAPF YAFUNGUA OFISI YA KANDA YA MAGHARIBI MKOANI GEITA


Naibu waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Josephat Sinkamba Akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Kushoto Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,Kulia Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw Eliud na wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Geita Mji Constatine Kanyasu wakikata utepe kwaajili ya kuzindua ofisi za LAPF kanda magharibi 
Naibu waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Josephat Sinkamba akiingia kwenye viwanja vya sherehe vya uzinduzi wa ofisi za kanda ya magharibi. 
Naibu waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Josephat Sinkamba ,akiwa pamoja na mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Hermani Kapufi na Meneja wa Kanda ya magharibi Vonnes Koka akimkaribisha Naibu waziri wa TAMISEMI. 
Wageni waalikwa wakifuatilia tukio 
Burudani zikiendelea kikundi cha Ngoma kutoka Mkoani Geita. 
Wageni waalikwa wakiwa wakifuatilia kwa makini burudani ya Ngoma. 

Jamaaa akionesha makeke yake kwa kula mchanga mwingi zaidi mdomoni. 
Meza Kuu ikiongozwa na Naibu waziri wa TAMISEMI. 
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akiwatambulisha baadhi ya watumishi na viongozi ambao walikuwa meza kuu. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola akitoa salaam za halmashauri ambayo anaiongoza. 
Mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akisalimiana na wananchi wakati wa zoezi la uzinduzi wa ofisi za kanda. 
Meneja wa Kanda ya magharibi Vonnes Koka akiwakaribisha wastaafu pamoja na wale ambao wanatakiwa kupewa fao la uzazi kwaajili ya kupatiwa hundi. 
Philip Ngika ni Mstaafu aliyestaafu hivi karibuni na kupatiwa mafao yake kiasi cha zaidi ya Milioni 72 na Naibu waziri wa TAMISEMI. 
Mwanachama wa LAPF ambaye amenufaika na fao la uzazi na kupatiwa kiasi cha zaidi ya Shilingi Laki sita 
Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw Eliud Sanga,Akimkabidhi Mgeni rasmi Naibu waziri wa TAMISEMI madawati miaka moja ambayo yametolewa kwenye halmashauri ya mji wa Geita. 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege akizungumza na Wanafunzi na kuwataka kusoma kwa bidii ili waje kufaulu masomo yao pindi watakapofika Darasa la Saba 
Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constatine Kanyasu akiomba halamshauri ya mji kupanishwa adhi ya kuwa Manispaa. 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege akiwa mbele ya jengo la LAPF
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Josephat Kandege akitembelea ofisi za LAPF 
Mgeni Rasmi naibu waziri wa nchi ofisi ya rais TAMISEMI akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa LAPF. PICHA NA JOEL MADUKANaibu waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Josephat Sinkamba ameziagiza halmashauri zinazodaiwa kwa kutokupeleka michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kutathmini kiasi wanachodaiwa na wakati wa maandalizi ya bajeti wahakikishe wanakwenda na mikakati ya kiasi walicholipa wanachodaiwa na namna ya kulipa madai kwenye mifuko hiyo.

Agizo hilo limetolewa leo wakati Bw Sinkamba akizindua ofisi za mfuko wa penisheni wa LAPF kanda ya magharibi ambayo itahudumia Mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita na Wilaya ya Sengerema na Halmashauri ya Buchosa.

Amesema miongoni mwa maeneo yanayodaiwa na mifuko ya hifadhi ni pamoja na watumishi wa Halmashauri hususani watendaji wa kata na vijiji na kwamba ni vema Halmashauri zikajua kiasi wanachodaiwa na kuandaa mikakati ya kulipa na kupeleka taarifa ya malipo kwa TAMISEMI.

Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw Eliud Sanga, ameeleza katika kuendelea kuboresha huduma ya mfuko huo wamekuwa wakilipa mafao mapema zaidi kwa mwanachama anayekaribia kustaafu na kwamba wamejidhatiti kutoa huduma bila usumbufu kwa wastaafu wanapohitaji mafao yao.Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amesema wanaamini kwa mashirika kuendelea kuweka ofisi za kanda ni njia mojawapo ya kukuza mji wa Geita na kufikia azma ya kuufanya mji huo kuwa Manispaa.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Bw Constantine Kanyasu amemuomba Naibu waziri wa TAMISEMI, Kuipandisha hadhi Halmashauri hiyo ili kuwa Manispaa kutokana na shughuli zilizopo kwenye Halmashauri hiyo kwa sasa.Mmoja wa wastaafu Bw Philip Ngika ameushukuru mfuko huo kwa namna unavyoendelea kuwajali wastaafu kwa kuwa yeye ni miongoni mwa watu wakaopatiwa mafao yao mapema zaidi.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment