Je uhusiano wa Diamond na Zari Hassan umefika ukingoni?


Msanii wa bongo fleva Diamond Platinumz na mpenziwe Zari HassanHaki miliki ya pichaDIAMOND PLATINUMZ
Image captionMsanii wa bongo fleva Diamond Platinumz na mpenziwe Zari Hassan
Inaonekana kana kwamba mapenzi kati ya mfanyibiashara Zari Hassan kutoka Uganda na mpenziwe nyota wa muziki wa bongo fleva Diamond Platinumz yanaelekea ukingoni.
Diamond ni baba ya watoto wawili wa Zari Hassan ambaye ameoenakana kunyamaza kwa muda baada ya mpenziwe Diamond kukiri hadharani kudanganya katika uhusiano wao na kupata mtoto na mwanamitindo wa Tanzania Hamisa Mobeto .
Tangu hilo litokee mambo hayajakuwa shwari kati ya hao wawili.
Ishara zaidi kwamba huenda mambo yamekwenda segemnege zilibainika wiki iliopita wakati Zari aliposhindwa kuhudhuria sherehe tatu zilizoandaliwa kusherehekea kuzaliwa kwa Diamond.
Zari alianza kwa kuondoka katika nyumba yake nchini Tanzania na kuelekea Afrika Kusini, kabla ya kuondoa picha za msanii huyo katika mtandao wake wa Instagram na akaunti nyengine za mitandao ya kijamii.
Lakini hakukomea hapo tu mbali na kuzifutilia mbali mbali picha zake alizopiga naye , Zari pia amemzuia katika mitandao yote ya kijamii ambapo Diamond hawezi kumuona.
Zari kwa sasa yuko Afrika Kusini kusimamia taasisi ya aliyekuwa mumewe Ivan Ssemwanga Brooklyn College na mali nyengine , huku akiendelea kulea watoto wake.
Mnamo tarehe 26 mwezi Septemba 2017 Zari aliandika katika mtandao wake wa facebook kwamba sijali kupoteza watu ambao hawataki kuwa katika maisha yangu.
Nimepoteza watu muhimu katika maisha yangu na bado naendelea kuishi vyema.
Hatahivyo haijulikani iwapo wapenzi hao wataonana wikendi hii kama kawaida.
Diamond ataelekea Uganda kuhudhuria sherehe za Carnival za mji wa Kampala.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment