Idadi ya watu waliouawa kwenye shambulizi Mogadishu yafika 300


Maandamano kushutumu al-Shabab Mogadishu, Somalia
Idadi ya watu waliouawa kwenye, mlipuko mkubwa wa bomu katika eneo lenye shughuli nyingi kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu siku ya Jumamosi, imefikia watu 300 hadi sasa, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Reuters
Takriban watu wengine 300 walijeruhiwa kwa mujibu wa AFP, wakati lori lililokuwa limejazwa vilipuzi lilipolipuka karibu na lango la hoteli.
Reuters walimnukuu Ahmed Ali, mwuguzi anayefanya kazi kwenye hospitali moja akisema kuwa miili 160 haikuweza kutambuliwa na hivyo ilizikwa na serikali jana.
Anasema kuwa miili mingine ilizikwa na jamaa zao.
Idadi ya watu waliouawa kwenye shambulizi Mogadishu yafika 300Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionIdadi ya watu waliouawa kwenye shambulizi Mogadishu yafika 300
Hilo ndilo shambulizi baya zaidi kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati zake mwaka 2007.
Rais Mohamed Abdullahi "Farmajo" Mohamed alilaumu kundi la al-Shabab kwa shambulizi hilo katili.
"Tumethibitisha kuwa watu 300 waliuawa kwenye mipuko huo. Idasi ya waliokufa huenda bado ikaongezeka na kuna watu kadha ambao bado hawajulikani waliko," Abdikadir Abdirahman, mkurugenzi wa idara ya magari ya kusafirisha wagonjwa aliliambia shiria la Reuters.
Idadi ya watu waliouawa kwenye shambulizi Mogadishu yafika 300Haki miliki ya pichaAFP
Watu waliandamana mogadishu kulaani shambulizi hiloHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWatu waliandamana Mogadishu kulaani shambulizi hilo
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment