CIA: Korea Kaskazini inakaribia kuwa hatari kwa Marekani


7 Machi 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKorea Kaskazini imezidisha kasi ya majaribio yake ya makombora miezi ya karibuni
Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA Mike Pompeo ametahadharisha kwamba Korea Kaskazini inakaribia sana kuwa na uwezo wa kuishambulia Marekani kwa kombora la nyuklia.
Amesisitiza kwamba taifa hilo bado linapendeleza zaidi kutumia diplomasia na vikwazo lakini amesema kwamba bado wanatafakari uwezekano wa kutumia nguvu za kijeshi.
Korea Kaskazini imekuwa ikidai kwamba tayari ina uwezo wa kuishambulia Marekani.
Hatua ya mwisho kwa Pyongyang
Pompeo ameambia mkutano wa Wakfu wa Uhifadhi wa Demokrasia mjini Washington kwamba "Korea Kaskazini sasa imekaribia sana kuwa na uwezo ambao kwa mujibu wa mtazamo wa kisera wa Marekani tunafaa kufanya vitendo vyetu tukizingatia kwamba wako karibu sana kufikisha lengo hilo."
"Wanapiga hatua sana, na sasa ni kufikiria tu jinsi ya kuwazuia kufika hatua ya mwisho."
Image captionBw Pompeo amesema Marekani bado inaweza kutumia nguvu za kijeshi
Ameonya kuwa ya Pyongyang imepiga hatua sana katika teknolojia yake ya makombora kiasi kwamba ni vigumu kwa majasusi wa Marekani kujua ni lini hasa watafanikiwa.
"Iwapo unazungumza kuhusu miezi kadha uwezo wetu wa kufahamu hilo kwa kina kwa sasa hauna maana kwa kiasi fulani," amesema.
Wikendi iliyopita, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson alisisitiza kwamba Rais Donald Trump angependa kutatua mzozo wake na Korea Kaskazini kupitia demokrasia.
Hiyo ni baada ya Bw Trump kumwambia hadharani kwamba asipoteze muda akitafuta mazungumzo na Kim Jong-un.

Mambo muhimu kuhusu hali ya kijeshi rasi ya Korea

SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment