Kampuni ya LG Electronics Yatoa Msaada wa Sare za Shule


Meneja Mkuu Masoko, wa kampuni ya LG Electronics, Tawi la Afrika Mashariki, Moses Marji (kulia) na Ofisa wa LG, Mohamed Ibrahim, wakimvisha sare mpya ya shule, mwanafunzi, Issa Abas, mwenye ulemavu wa ngozi, albinism katika Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko jiji Dar es Salaam, jana, wakati kampuni hiyo ya LG Electronics imetoa msaada wa sare za shule kwa Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko kama sehemu ya Wajibu wa Jamii wa Kampuni kwa lengo la kusaidia watoto wenye ulemavu nchini Tanzania, kufuatia shule hiyo ya Uhuru Mchanganyiko kukabiliwa na changamoto mbalimbali katika kuwaelimisha watoto wenye ulemavu ambao wana mahitaji maalum.
Meneja Mkuu Masoko, wa kampuni ya LG Electronics, Tawi la Afrika Mashariki, Moses Marji (kulia) na Ofisa wa LG, Mohamed Ibrahim, wakimvisha sare mpya ya shule, mwanafunzi, Kelvin Joseph, mwenye ulemavu wa kutosikia, katika Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko jiji Dar es Salaam, jana, wakati kampuni hiyo ya LG Electronics imetoa msaada wa sare za shule kwa Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko kama sehemu ya Wajibu wa Jamii wa Kampuni kwa lengo la kusaidia watoto wenye ulemavu nchini Tanzania, kufuatia shule hiyo ya Uhuru Mchanganyiko kukabiliwa na changamoto mbalimbali katika kuwaelimisha watoto wenye ulemavu ambao wana mahitaji maalum.
Meneja Mkuu Masoko, wa kampuni ya LG Electronics, Tawi la Afrika Mashariki, Moses Marji (katikati mwenye kofia) , katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko jiji Dar es Salaam, jana, wakati kampuni hiyo ya LG Electronics imetoa msaada wa sare za shule kwa Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko kama sehemu ya Wajibu wa Jamii wa Kampuni kwa lengo la kusaidia watoto wenye ulemavu nchini Tanzania, kufuatia shule hiyo ya Uhuru Mchanganyiko kukabiliwa na changamoto mbalimbali katika kuwaelimisha watoto wenye ulemavu ambao wana mahitaji maalum.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam, Mwal. Anna Mshana, akikabidhi sare za shule kwa Mwalimu Abdalah Ahamed, baada ya kampuni ya LG Electronics kutoa msaada wa sare za shule kwa Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko kama sehemu ya Wajibu kwa Jamii wa Kampuni hiyo, kwa lengo la kusaidia watoto wenye ulemavu nchini Tanzania, kufuatia shule hiyo ya Uhuru Mchanganyiko kukabiliwa na changamoto mbalimbali katika kuwaelimisha watoto wenye ulemavu ambao wana mahitaji maalum. Wanaoshuhudia ni Meneja Mkuu Masoko, wa kampuni ya LG Electronics, Tawi la Afrika Mashariki, Moses Marji (katikati mwenye kofia) na wanafunzi wa shule hiyo.


Kampuni ya  LG Electronics ya Africa Mashariki,   imetoa msaada wa sare za shule  kwa  Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko kama sehemu ya utekelezaji  Wajibu wa Jamii wa  Kampuni  hiyo kwa  lengo la kusaidia watoto wenye ulemavu na mahitaji maalum nchini Tanzania.

Msaada huo, umekabidhiwa na  Meneja Mkuu Masoko, wa LG Electronics East Africa,  Moses Marji katika halfa fupi iliyofanyika shiuleni hapo jana, na kuhudhuriwa na  wawakilishi wa serikali, waalimu na wanafunzi wa shule hiyo. Bw. Murji amesema LG imeamua kutoa msaada huo kwa Shule ya Uhuru Mchanganyiko kwa kuwa shule hiyo ina jukumu muhimu katika kusaidia watoto wenye ulemavu huku ikikabiliwa na changamoto mbalimbali katika kukidhi mahitaji ya mwanafunzi hao wenye mahitaji maalum.

Amesema LG Electronics ina utamaduni wa kutumikia jamii zinazowazunguka, kwa kutoa misaada mbalimbali kusaidia jamii  ambapo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, LG Electronics imekuwa imesaidia watu wanaoishi na ulemavu kupata viungo vya bandia pamoja na kujenga uelewa juu ya shida ya watu wenye ulemavu kwa njia ya ushirikiano wao na Hospitali ya PCEA Kikuyu nchini Kenya, mamia ya watu wenye ulemavu wa viungo,  wan chi za Afrika Mashariki, wamefaidika kwa kupatiwa miguu ya bandia wakiwemo waTanzania walio faidika na mpango huu.

Mwakilishi wa  Manispaa wa Ilala, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Bw. Muna Roberts,  ameshukuru kampuni ya LG Electronics,  kwa msaada huo kwa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, na kuelezea msaada huo ni kuisaidia serikali ya Tanzania kuipunguzia mzigo wa kuihudumia shule hiyo ya serikali, hivyo wameisaidia serikali, ana ametoa wito kwa  taasisi nyingine kufanya hivyo, kwa kusaidia watoto wenye ulemavu ambao wana mahitaji maalum, serikali peke yake haiwezi kukidhi kila kitu.

Akipokea  mchango huo, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Uhuru Mchanganyiko, Mwalimu Anna Mshana, aliishukuru LG Electronics, kwa msaada huo wa  sare kwa shule yake, na kusema shule hiyo inajumuisha watoto wenye aina tofauti ya ulemavu, wakiwemo wasioona, wasio sikia, wenye ulemavu wa viungo, wenye ulemavu wa ngozi, na wenye mtindio wa ubongo,  amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 650 ambao asilimia 25% ni wanafunzi wenye ulemavu, wenginde ni wanafunzi wa Bweni, na wengine ni wa kutwa.

Mwalimu Mshana amesema,  wengi wa wanafunzi wa shule hiyo ni  kutoka kwa familia masikini hivyo shule hiyo haitozi ada  hiyo inategemea zaidi kuhudumiwa na serikali na misaada ya Wasamaria wema hivyo ameziomba taasisi nyingine kujitokeza kuisaidia shule hiyo yenye changamoto nyingi kuhudumia watoto wenye ulemavu ambao wana mahitaji maalum.

Amesema shule hiyo ina mahitaji mengi muhimu yanayo hitaji msaada kutoka kwa jamii, kama vile vifaa vya kujifunzia kwa watoto wenye ulemavu, inahitaji kupanua maabara yake ya kompyuta na inahitaji kompyuta zaidi kwa mahitaji maalum kama kompyuta kwa vipofu, na kwa viziwi .

Kwa upande wao, wanafunzi, Issa Abasi anaewakilisha wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi,  albino, Lydia Issack anayewakilisha wanafunzi wenye ulemavu wa kutosikia,  na  Kevin Joseph akiwakilisha wanafunzi wasioona, wote walishukuru LG Electronics East Africa kwa misaada huo wa sare, za shule na kuomba na taasisi nyingine ziige mfano huo, kujitokeza kuwasaidia.
Kuhusu LG Electronics, Inc.

LG Electronics, Inc,  ni mvumbuzi anayeongoza kimataifa katika teknolojia katika vifaa vinavyotumia umeme ,simu za mkononi na vifaa vya nyumbani, imeajiri watu 75,000 wanaofanya kazi katika vituo 118 vya kazi duniani kote . Ikiwemo mauzo ya kimataifa ya dola za kimarekani  47.9 bilioni mwaka 2016, LG inaendesha michepuo minne ya biashara ― Vifaa vya nyumbani & udhibiti hewa , mawasiliano, Burudani za nyumbani na vifaa vya magari  ― na ni moja ya wazalishaji wanaoongoza wa Luninga bapa , Simu za mkononi ,viyoyozi, mashine za kufulia na majokofu . Kwa habari zaidi na taarifa kuhusu bidhaa za LG , tafadhali tembelea  www.LGnewsroom.com
SHARE

 • Image
 • Image
 • Image
 • Image
 • Image
  Blogger Comment
  Facebook Comment

4 comments:

 1. In the event that you experience a daily paper promotion or sale site, you'll be fortunate to discover somebody who's even inspired by your stuff.est soldering iron

  ReplyDelete
 2. Likewise, if there should be an occurrence of a crisis, one ought to dependably bring in for help and be wary not to go close to the machines.my company

  ReplyDelete
 3. You can get things done to endeavor to help the electronics to not produce such a great amount of warmth in any case.adlist24.com

  ReplyDelete
 4. Electronics and electrical types of gear are an imperative and unavoidable piece of everyday lives. Feedster Entrpreneur News

  ReplyDelete