TaGEDO YAPATA UGENI KUTOKA UJERUMANI, WAFANYA SHUGHULI MBALIMBALI IKIWEMO USAFI WA MAZINGIRA

Vijana wa Kituo cha ubunivu na ushonaji nguo cha Taasisi ya Kijamii ya TaGEDO, wakimwelekeza jinsi ya kutumia cherehani, kijana Astrid Naundorf kutoka Chuo Kikuu Cha Munister, wakati vijana wa Chuo hicho walipotembelea Kituo hicho, Kigamboni Dar es Salaam, leo.
---------------------------------------


KIGAMBONI, DAR ES SALAAM.

Vijana kutoka Chuo Cha  Munister nchini Ujerumani, leo wametembelea Kituo cha Taasisi ya Kijamii ya kuelendeleza Vijana na Kinamama katika Ujasiriamali hapa nchini (TaGEDO) kilichopo Kigamboni Dar es Salaam, na kushiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo kusafisha mazingira.

Vijana hao zaidi ya 20 walishirikiana na vijana wenzao kutoka TaGEDO na kufanya usafi kwenye eneo la Ofisi ya Mtaa wa  Kisiwani na baadaye kushiriki katika mafunzo ya ushonaji nguo kwenye mradi wa ushonaji nguo wa kituo hicho na baadaye ulifanyika mjadala wa kubadilishana uzoefu katika mafanikio na changamoto zinazokabili vijana na kinamama.

Kituo hicho cha Taasisi ya TaDEDO hadi sasa kina vijana 83 ambao kwa namna mojawapo walikosa fursa  ikiwemo ya kutoendelea na masomo ambao sasa wanapatiwa mafunzo ya ujasiriamali wa kubuni na kushona nguo ambapo baadhi yao tayari ni mafundi.

Akizungumzia kituo hicho, Kiongozi wa TaGEDO Venance Kalumanga, amesema lengo la kuanzisha mafunzo hayo ya kubuni na kushona mavazi ni kutaka baadaye waanzishe kiwanda kikubwa cha ushonaji kitakachoweza kutoa ajira kwa kina mama na vijana ikiwa ni moja ya hatua ya kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli katika azma yake ya kuifanya Tanzania kuwa ya uchumi wa Viwanda.

"Hadi sasa kwenye kituo chetu tunazo cherehani kumi ambazo baadhi tulijitolewa sisi waanzilishi ambao tunatoka Chuo Cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni na nyingine tulipewa na mfadhili kutoka Chuo Kikuu cha Munster cha Ujerumani, Dk. Reinhold Hemker. Sasa kwa kuwa mafunzo tunaoa bure kwa vijana na kina mama wanaokuja hapa changamoto ni namna ya kukidhi mahitaji, hivyo tunawaomba wadau wote wa maendeleo wajitolee kutusaidia ili tulisaidie taifa letu kwa ufanisi", alisema Kalumanga.

Kalumanga ambaye ni Mhadhiri katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, katika Idara ya Jinsia na Maendeleo, alisema, baadhi ya wadau ambao pia wametoa mchango mkubwa kuanzishwa TaGEDO ni pamoja na wa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na UDOM.
 Taasisi ya Kijamii ya kuelendeleza Vijana na Kinamama katika Ujasiriamali hapa nchini (TaGEDO) Venance Kalumanga akichoma taka, wakati yeye na wenzake wa Taasisi hiyo, walipoungana na Vijana kutoka Chuo Cha  Munister nchini Ujerumani, kufanya usafi kwenye eneo la Ofisi ya Mtaa wa Kisiwani, Kigamboni, dar es Salaam, leo
 Vijana wa TaGEDO wakishirikiana na Vijana hao kutoka Ujerumani kukusanya taka wakati wakifanya usafi kwenye ofisi ya Mtaa wa Kisiwani, Kigamboni Dar es Salaam, leo.
ZIFUATAZO NI PICHA TAGEDO NA VIJANA HAO KUTOKA UJERUMANI WAKISHIRIKI KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI WAKATI WA ZIARA HIYO, LEO
🔻
 MSAFARA KUTOKA MTAA WA KISIWANI KWENDA OFISI YA TaGEDO
🔻
 MAANDALIZI YA CHAKULA CHA WENYEJI NA WAGENI
🔻
MAFUNZO YA USHONAJI
🔻
 MAFUNZO YA USHONAJI
🔻
 CHAKULA CHA MCHANA
🔻
 PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment