Korea Kaskazini yaionya Marekani kufuatia vikwazo vya UN


South Korean soldiers stand guard before North Korea's Panmon Hall (rear C) and the military demarcation line separating North and South Korea, at Panmunjom, on 6 AugustHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMsukosuko unaendelea wakati Korea Kaskazini inaendelea na majaribio ya makombora

Korea Kaskazini yaionya Marekani kufuatia vikwazo vya UN

Korea Kaskazini imeapa kulipiza kisasi na kuhakikisha kuwa Marekani imelipia gharama, kwa kubuni vikwazo vya Umoja wa Mataiafa kufuatia na mpango wake wa silaha za nuklia.
Vikwazo hivyo vilivyoungwa mkono kwa kura nyingi na Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi "ni ukiukaji ya uhuru wa nchi," shirika la serikali la habari la Korea Kaskazini KCNA lilisema.
Members of the United Nations Security Council vote on a resolution to implement new sanctions against North Korea at United Nations headquarters in New York, 5 August 2017Haki miliki ya pichaEPA
Image captionAzimio hilo lilipitishwa kwa kura 15 kwa sufuri
Kwa upande mwingine Korea Kusini inasema kuwa Korea Kaskazini imekataa ombi la kutaka wafanye mazungumzo.
Vikwazo hivyo vililenga kuzuia mauzo ya bidhaa za Korea Kaskazini kwa theluthi moja.
Vikwazo hivyo vya Umoja wa Mataifa vilifuatia majaribio ya mara kwa mara ya makombora yanayofanywa na Marekani, hali ambayo imeuzua wasi wasi kwenye rasi Korea.
Missile launchHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKombora la Korea Kaskazini
Leo Jumatatu Korea Kaskazini ilisema kuwa itaendelea na mpango wake wenye utata wa kuunda zana za nuklia.
Kupitia kituo cha habari cha serikali cha KCNA, Korea Kaskazini ilisema kuwa haiwezi kuachana na mpango wake wakati inakabiliwa na vitisho kutoka Marekani.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment