Wavenezuela waitikia wito wa mgomo


Mitaa mingi ya Caracas ilikuwa mitupuHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMitaa mingi ya Caracas ilikuwa mitupu

Wavenezuela waitikia wito wa mgomo

Mamilioni ya Wavenezuela wameitikia wito wa Upinzani wa kubakia nyumbani, katika mgomo wa kwanza wa saa 24 kufanyika nchini humo kwa zaidi ya muongo mmoja.
Hatua hiyo ni kupinga mipango ya serikali ya kuandika tena katiba mpya.
Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi katika miji kadhaa, walipopambana na waandamanaji.
Polisi walipambana na WaandamanajiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPolisi walipambana na Waandamanaji
Katika ghasia hizo waandamanaji watatu waliuawa.
Hata hivyo, katika maeneo yanayounga mkono serikali ya nchi hiyo mjini Caracas, maisha yaliendelea kama kawaida.
Katika hotuba yake kupitia televisheni, Rais Nicolas Maduro amesema mamia ya wafanyabiashara waliendelea na shughuli zao kama kawaida na kwamba viongozi wa mgomo huo watakamatwa.
Lakini upinzani nao umedai kuwa Rais Maduro anajaribu kujiimarisha madarakani kwa kubadili katiba, hali ambayo itabadili hali ya sasa ya upinzani kudhibiti bunge.
Na katika Umoja wa Mataifa mwanadiplomasia wa Venezuela amejiuzulu katika kupinga hatua zinazochukuliwa na serikali yake.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment