Ufyatuaji risasi watokea kwenye ubalozi wa Israel nchini Jordan


Security forces stand guard outside the Israeli embassy in the residential Rabiyeh neighbourhood of the Jordanian capital Amman following an "incident" on July 23, 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionVikosi vya usalama vimefunga barabara eneo hilo

Ufyatuaji risasi watokea kwenye ubalozi wa Israel nchini Jordan

Watu wawili raia wa Jordan wameuawa na muisrael mmoja kujeruhiwa wakati wa kisa cha ufyatuaji risasi kwenye ubalozi wa Israel katika mji mkuu wa Jordan Amman.
Watu hao walikuwa wakifanya kazi na kampuni moja ya zamani na waliingia ndani ya ubalozi kabla ya ufyatuaji risasi kuanza kwa mujibu wa polisi.
Ripoti chache zimetolewa kuhusu kile kilisababisha kutokea kwa ufyatuaji huo wa risasi.
Vikosi vya usalama vimezingira ubalozi huo na utawala wa Israel umewahamisha wafanyakazi.
Ufyatuaji huo ulitokea katika jengo moja linalotumiwa na ubalozi wa Israel.
Mamlaka za Israel hazijazungumzia kisa hicho.
Ubalozi huo wenye ulinzi mkali uko mtaa wa Rabiyeh ambalo ambao ni wa kifahari mjini Amman.
Siku ya Ijumaa maelfu ya watu waliandamaa mjini Amman kupinga hatua ya Israeal ya kuweka vifaa vya kutambua chuma katika aneo takatifu kwa waislamu na wakiristo mashariki mwa Jerusalem.
A general view of the city of Amman at twilight on March 26, 2013 in Amman, Jordan.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRipoti chache zimetolewa kuhusu kile kilisababisha kutokea kwa ufyatuaji huo wa risasi.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment