Trump achapisha video 'akiipiga' CNNA screenshot of the president's tweetHaki miliki ya pichaTWITTER
Image captionVideo hiyo inaonekana kuchapishwa katika mtandao wenye kumpendelea Trump mapema wiki hii.
Rais wa Marekani Donald Trump amechapisha video katika mtandao wa Twitter ikimuonyesha akimpiga mtu aliye na nembo kichwani ya shirika la habari la CNN.
Video hiyo iliyofanyiwa ukarabati ni ile inayomuonyesha Trump wakati alihudhuria michezo ya mieleka ya WWE mwaka 2007, ambapo 'alimshambulia' mmiliki wa michezo hiyo Vince McMahon.
Video hiyo inaonekana kuchapishwa katika mtandao wenye kumpendelea Trump mapema wiki hii.
CNN baadaye ilimlaumu Rais kwa kuibua ghasia dhidi ya vyombo vya habari.
Donald Trump gets taken to the mat by 'Stone Cold' Steve Austin after the the Battle of the Billionaires at the 2007 World Wrestling Entertainment's Wrestlemania April 1, 2007 at Ford Field in Detroit, Michigan.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionVideo hiyo inaonekana kuchapishwa katika mtandao wenye kumpendelea Trump mapema wiki hii.
Mchambuzi mmoja katika kituo cha ABC Ana Navarro, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa Trump, alisema kuwa video hiyo ni uchochezi na huenda ikasababisha mwandishi kuuliwa.
Lakini mshauri wa masuala ya usalama nchini Marekani Thomas Bosset, ambaye awali alihojiwa na kituo cha ABC alisema video hiyo haionekani kuwa tisho.
Mara kwa mara Rais Trump amekuwa kwenye mzozo na kituo cha CNN anachokiita 'taarifa bandia'
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment