Qatar kudai fidia kutoka nchi zilizoitenga


Mji mkuu wa Qatar DohaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMji mkuu wa Qatar Doha
Nchi ya Ghuba ya Qatar imesema itadai fidia dhidi ya nchi zake jirani zilizoitenga nchi hiyo hasa kiuchumi.
Nchi za Saudi Arabia, UAE, Bahrain na Misri zote zimekata mahusiano ya anga, ardhi na bahari na Qatar baada ya kuishutumu kuunga mkono makundi ya kigaidi.
Qatar imekana madai hayo, na imeunda tume itakayoshughulikia malalamiko ya hasara iliyopatikana kwa kampuni zake pamoja na watu binafsi.
Walalamikaji hao wanaweza kuwemo shirika la ndege la taifa, ambalo limebidi kubadili njia licha ya awali kutumia anga za nchi jirani.
Qatar kudai fidia kutoka nchi zilizoitengaHaki miliki ya pichaEMPICS
Image captionQatar kudai fidia kutoka nchi zilizoitenga
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment