Makaburi ya halaiki yagunduliwa DRC


DRC
Image captionRais Joseph Kabila

Makaburi ya halaiki yagunduliwa DRC

Umoja wa mataifa umesema kwamba umetambua makaburi makubwa zaidi ya thelathini na nane kutokana na vurugu za hivi karibuni nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo .
Na kusema kwamba uvumbuzi huo unaweza kusababisha utambuzi wa makaburi mengine zaidi kama ambavyo yaliyowahi kutambuliwa jimboni Kasai ya Kati yapatayo themanini.
Inaelezwa kuwa watu zaidi ya elfu tatu wameuawa na zaidi ya milioni kukosa makaazi yao kufuatia mapigano yanayoendelea katika eneo hilo ambayo yaliibuka baada ya kuuawa kwa kiongozi wa kijeshi mwezi August mwaka jana.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imerusha mzigo wa lawama kwa kikundi cha kijeshi cha Kamuina Nsapu kuhusika na makaburi hayo ya halaiki.
Ingawa mashuhuda wa mambo nchini humo wanaarifu kuwa wameshuhudia magari ya kijeshi yakirusha maiti ardhini.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment