Madonna azuia mnada wa barua ya uhusiano wake na Tupac Shakur


Madonna na Tupac Shakur kuliaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMadonna na Tupac Shakur kulia

Madonna azuia mnada wa barua ya uhusiano wake na Tupac Shakur

Jaji mmoja nchini Marekani amesitisha mnada wa vitu binafsi vya mwanamuziki Madonna baada ya kusema kuwa haki yake ya faragha ilikiukwa.
Jaji wa mji wa New York Gerlad Lebovits aliamuru kesi hiyo kusikizwa kikamilifu mnamo mwezi Septemba tarehe 6, akilizuia jumba litakalofanya mnada huo la Gotta have Rock kuendelea na biashara hiyo.
Chupi ya Madonna, kitabu cha hundi , kichana , picha na barua ya uhusiano kati ya msanii huyo na aliyekuwa mwanamuziki Tupac Shakur ni miongoni mwa vitu vilivyosimamishwa kupigwa mnada.
Madonna anasema kuwa vitu hivyo viliibwa na rafikiye wa zamani.
Barua hiyo ya Tupac ambapo Tupac anasema kuwa uhusiano wake na Madonna ulivunjika kutokana na ubaguzi wa rangi ilitarajiwa kuuzwa kwa dola 400,000.
Barua ya Tupac Shakur aliyomwandikia madonna akiwa jelaHaki miliki ya pichaGOTTA HAVE ROCK AND ROLL/PA WIRE
Image captionBarua ya Tupac Shakur aliyomwandikia madonna akiwa jela
Barua hiyo ni ya tarehe 15 mwezi Januari 1995 na iliandikwa na Tupac Shakur wakati alipokuwa akihudumia kifungo cha miezi 18 kabla ya kupigwa risasi na kuuawa.
Wasanii wote wawili walikuwa maarufu sana wakati huo.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment