Waislamu wametakiwa kuendeleza Ucha Mungu na mema waliyokuwa wakiyafanya katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Waislamu wametakiwa kuendeleza Ucha Mungu na mema waliyokuwa wakiyafanya katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Sheikh Yussuf Mecca, kutoka Columbus, Ohio

Wito huo ulitolewa jana na Sheikh Yussuf Mecca alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Iddi zilizoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu wa Tanzania wa Jiji la Washington na Vitongoji vyake ijulikanayo kwa jina la TAMCO.
"Kwa vile mwezi wa Ramadhani umekwisha isiwe yale yote mazuri tuliyokuwa tunayafanya ikawa ndiyo basi, na tusubiri Ramadhani nyengine" alisema Sheikh Yussuf.
Aliendelea kusisitiza umuhimu wa kujitahidi kumcha Mungu wakati wowote na kujitahidi katika kutenda mambo mema na ibada ili kujiandaa na safari ya Akhera ambayo inanaweza kumfikia mtu wakati wowote.
" Hakuna hata mmoja ambaye anajua ni siku gani atafumba jicho na atakufa", alisisitiza Mgeni huyo rasmi kwenye shere hizo, huku akitilia nguvu hoja yake kwa Aya ya Qur'an isemayo: "كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ" (Kila nafsi itaonja mauti/kifo), akigogoteza kuwa hakuna mtu yoyote anayejua atakufa lini au mahali gani.
Aliongeza kusema kuwa kurejea kwenye maasi baada ya juhudi kubwa za ucha Mungu na ibada katika mwezi wa Ramdhani ni sawa na kuiharibu kazi ya kiufundi liyofumwa kwa juhudi na ustadi mkubwa.
Mwenyekiti wa TAMCO Bwana Ali Muhammed
Sherehe za Iddi za Waislamu wa Tanzania katika Mji huo Mkuu wa Marekani, ni utamaduni ulioanza tangu mwaka 1998, ambapo Waislamu waliona haja ya kuwa na mjumuiko wa pamoja katika Siku Kuu, ikizingitwa kuwa Marekani si nchi ya Kiislamu na kwa hivyo hakuna sherehe rasmi za Iddi, kama alivyoelezea Mwenyekiti wa TAMCO Bwana Ali Muhammed:
"Wazee na vijana waliokuwepo hapa katika miaka hiyo waliona kuna haja ya kuanzisha Umoja ambao utawasaidia katika mambo yao ya Kidini, siyo tu kwenye sherehe za Iddi, bali pia katika maswala mengine ya sherehe na misiba. Na baada ya chombo hicho kuanzishwa ndipo ukaanza utaratibu wa kuandaa sherhe kama hizi za Iddi".
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment