Oman yapeleka chakula Qatar


Baadhi ya makontena yaliyobeba vyakula katika bandari ya Oman
Image captionBaadhi ya makontena yaliyobeba vyakula katika bandari ya Oman
Nchi ya Qatar imefungua huduma za usafiri wa meli kutokea Oman kwa lengo la kukabiliana na vikwazo vya usafiri vilivyowekwa na majirani zake.
Meli kadhaa zikiwa zimebeba vyakula na bidhaa mbalimbali zimeonekana zikielekea Qatar kutokea bandari mbili zilizopo Oman.
Qatar inategemea uingizwaji wa chakula kutoka nje.
Saudi Arabia, Bahrain na muungano wa Falme za Kiarabu zilizuia uingizwaji wa bidhaa kwenda Qatar wiki chache zilizopita kwa shutuma kuwa nchi hiyo inaunga mkono vitendo vya kigaidi.
Waziri wa mambo ya nje wa Qatar amewasili mjini London na kisha Paris kujadili mgogoro huo.
Qatar huagiza asilimia kubwa ya chakula chake kutoka nchi za nje
Image captionQatar huagiza asilimia kubwa ya chakula chake kutoka nchi za nje
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment