Matokeo ya Uchaguzi 2017 kwa kifupi: Maeneo muhimu kwa mtazamo


Matokeo hayo yakingaa juu ya Jumba la Habari - bbc
Image captionMatokeo yaliyobashiriwa ya baada ya upigaji kura kwenye Jumba la habari la BBC
Huku zaidi ya matokea 100 yakiwasilishwa, shirika la habari la BBC, imeelezea utabiri wake, kuhusiana na matokeo ya mwisho. Inatabiri viti 322 vitanyakuliwa na chama cha Conservatives, kiwango chini kwa viti 9 ikilinganishwa na 2015, viti 261 kwa Labour - juu kwa viti 29, viti 32 kwa chama cha SNP, hasara ya viti 24.
Chama cha Lib Dems vitaongezeka kwa viti vitano zaidi na kufikia viti 13, Plaid Cymru kikisalia na viti 3 tu. Greens kikiwa na kimoja tu, ilihali kile cha UKIP kikiwa bila na viti 18 kwa vyama hivyo vingine. Matokeo ya utafiti wa baada ya uchaguzi wa BBC, ITV na Sky yanaonesha hakuna chama kitakachopata wingi wa wabunge katika Bunge la Commons.
Inaashiria kuwa, chama cha Conservatives kitaimarika kwa kiasi fulani, kuliko ilivyotabiriwa kwenye matokeo yaliyobashiriwa ya baada ya upigaji kura, lakini kitamaliza chini kidogo nyuma ya washindi.
BBC yakuletea moja kwa moja matokeo ya uchaguzi mkuu UingerezaHaki miliki ya pichaPA
Image captionBBC yakuletea moja kwa moja matokeo ya uchaguzi mkuu Uingereza
Inaonekana kama chama cha Labour kinafanya vizuri ambapo zaidi ya asilimia 55% ya wapigaji kura walitaka kusalia ndani ya EU, huku kukiwa na asilimia 8% ya kura katika maeneo ya kushindaniwa kwa Labour katika maeneo hayo, anasema mtaalamu wa maswala ya kisiasa Profesa John Curtice. Kwa tofauti, kuna asilimia 1% ya kura ya kushindaniwa kwa chama cha Conservatives katika maeneo ambayo wanaotaka Uingereza kuondoka ndani ya muungano wa Eu (leave) walishinda kwa asilimia 60%.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment