KONGAMANO LA PILI LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI LAFANYIKA MKOANI DODOMA LEO


 Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dkt.  Jim Yonazi akijibu hoja mbalimbali ambazo ziliibuliwa katika kongamano la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika leo mjini Dodoma . TSNwalikuwa mmoja wa wadhamini. Dk Yonazi alisema kuwa ili kuwaezesha wananchi kiuchumi ni lazima jamii ihabarishwe juu ya fursa mbalimbali zilizopo, lakini pia muhimu wa sekta binafsi kuwa na ubunifu na mifumo ya kujitengenezea utajiri.Picha zote na Mroki Mroki-dailynewstzonline.blog

Afisa Mtendaji Mkuu wa MM Maxcom , Juma Rajab akielezea uzoefu wake na kusema kuwa inahitajika kuwawezesha wajasiriamali wote, wadogo, wa kati na wakubwa ili kufanikisha wananchi kuweza kuingia katika uchumi wa viwanda.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akitoa mada juu ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ambapo alisema ni vyema viongozi na jamii ikawana na utaratibu wa kuchapa kazi ili iweze kufanikiwa katika suala la uwezeshaji wananchi kiuchumi.

 Wakuu wa Mikoa waliohudhuria Kongamano hilo.
 Wadau wa Kongamano hilo kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) nao walikuwepo. TSN ilikuwa moja ya wadhamini.
 washiriki wa Kongamano
 Wakuu wa Mikoa Mbeya, Amos Makala (kulia) na John Mongela wakifuatilia kongamano hilo
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment