KIJANA ABDULMJID MUJAHID KUTOKA YEMEN AMEIBUKA MSHINDI WA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA QUR-AN


KIJANA Abdulmjid Mujahid kutoka Yemen ameibuka mshindi wa mashindano ya kimataifa ya Qur-an yaliyozishindanisha nchi kumi ambapo mshindi  amezawadiwa dola 5000 za kimarekani huku ubalozi wa Kuwait ukimzawadia dola 500, mshindi wa pili wa mashindano hayo ni Omary Abdallah kutoka Tanzania ambaye nae amezawadiwa dola 4000 na dola 300 kutoka ubalozi wa Kuwait.

Mashindano hayo yameshirikisha nchi kumi zikiwemo Uganda, Mali, Tanzania Bara, Yemen, Russia, Uingereza, Libya, Bangladesh, Marekani na Jumuiya ya Falme za kiarabu (United Arab Emirates).
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akimkabidhi hundi ya dola za Kimareni 5,000 mshindi kwanza wa mashindano ya kimataifa ya Qur-an Abdulmjid Mujahid kutoka Yemen leo jijini Dar es Salaam. 

Pia Mashindano hayo yameudhuriwa na viongozi mbalimbali yakiongozwa na makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddy, na mlezi wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi, Muft Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuber, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum, mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete na mgeni maalum kutoka Saudi Arabia Abdallah Basfar ambaye ni msomaji Qur-an wa kimataifa.

Akihutubia katika mashindano hayo Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Ally Seif Iddy ameeleza kuwa vijana wamekosa adabu na matendo ya ulawiti, mauaji kwa watoto wachanga, unyanyasaji, mauaji ya wenye ulemavu wa ngozi yamekuwa yakiripotiwa, huku akieleza kuwa aamini kama Mwenyezi Mungu anayaridhia matendo haya, hivyo tabia za watanzania na waislamu ziendane na maamrisho ya Qur-an.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akimkabidhi hundi ya dola za Kimareni 4,000 mshindi pili wa mashindano ya kimataifa ya Qur-an wa Tanzania,Omary Abdallah leo jijini Dar es Salaam. 

Pia Makamu wa Rais Balozi Seif Ally Iddy ameongeza kuwa mbora ni mwenye kujifunza Qur-an na akawafundisha wengine Mwenyezi Mungu amewanasihi waislamu katika kitabu chake kitukufu.

Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi awapongeza wanafunzi wa kiislamu wanaojifunza Qur-an kwani kufanya hivyo ni kuiendea jamii njema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Tanzania Sheikh Othman Ally Kaporo amewataka wadau wa masuala ya Qur-an kuhakikisha Qur-an inakaa katika nyoyo za vijana ili jamii iweze kuwa bora na kuheshimiana wakubwa kwa wadogo.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi, akipokea tuzo ya heshima kutoka Muft wa Tanzania Abubakar Zuber iliyotolewa na Jumuiya ya kuhifadhisha Qur-an Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo.

Huku Muft Mkuu wa Tanzania Abubakari  amesema ni vyema watu wakajifunza Qur-an kwasababu ni dawa ya kila tatizo, endapo waja wataifuata kwa mafunzo yaliyoamrishwa na kuacha yaliyokatazwa, kwani Qur-an imekataza kuuana, kuchukiana, kuvuruga amani.

Jumuiya ya kuhifadhisha Qur-an imetoa tuzo za heshima kwa wanahakati wa Qur-an akiwemo Abdallah Basfar na Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi, huku ikitambua mchango huo kwa masheikh mbalimbali akiwemo Sheikh Ismail Mohammed, Sheikh Adam Ahmad, Marehemu Hashim Haji, Isihaka Abdehell, Marehemu Yahya Hussein na Sheikh Mohammed.

Mashindano hayo yameanzishwa 1992 yakiwa yakimkoa na mpaka sasa ni mashindano ya kimataifa huku yakiwa niya 25 tangu kuanzishwa kwake.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi, akizungumza katika mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd, akizungumza katika mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo.
Muft Mkuu wa Tanzania Abbakar Zubeir akizungumza katika katika mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya pamoja

Sehemu ya viongozi mbalimbali na wananchi wakifatilia mashindano haoyo leo jijini Dar es Salaam.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment