Helikopta ya polisi yashambulia mahakama ya juu Venezuela


Venezuelan authorities inspect the area around the Supreme Court in Caracas, Venezuela, 27 June 2017Haki miliki ya pichaEPA
Image captionPolisi ambaye alidaiwa kuiendesha ndege hiyo ya polisi iliyokuwa imeibwa alitoa taarifa ya kupinga serikalia
Mahakama ya juu nchini Venezuela imeshambuliwa kwa maguruneti yaliyorushwa kutoka kwa helkopta katika kile rais Nicolas Maduro amekitaja kuwa shambulizi la kigaidi.
Picha katika mitandao ya kijamii zilionyesha helikopta ya polisi ikizunguka mjini kabla ya milio ya risasi na milipuko kusikika.
Polisi ambaye alidaiwa kuiendesha ndege hiyo ya polisi iliyokuwa imeibwa alitoa taarifa ya kupinga serikalia. Hadi sasa hajulikani aliko.
Kisa hiki kinajiri baada ya maandamano makubwa kupinga matatizo ya kisiasa na kiuchumi nchini humo.
Man identifying himself as Oscar PĂ©rez makes statementHaki miliki ya pichaINSTAGRAM
Image captionPolisi huyo alijitambua kama Oscar Perez kupitia video iliyochapishwa kwenyr mtandao wa Instagram.
Mahakama ya juu mara nyingi hukosolewa na upinzani kwa maamuzi yake ya kuchangia bwana Maduro kusalia madarakani.
Akitoa hotuba kutoka kwa ikulu, Rais Maduro alisema kuwa helikopta ilipita juu ya mahakama ya juu na pia kwenye wizara ya sheria na ile ya mambo ya ndani.
Maafisa wanne walionukuliwa na shirika la Reuters, walisema kuwa maguruneti manne yaliangushwa kwenye mahakama na risasi 15 kufuytuliwa kuenda kwa wizara ya mambo ya ndani.
Handout photo shows Venezuelan President, Nicolas Maduro (C), during a rally of supporters in Caracas, Venezuela, 27 June 2017Haki miliki ya pichaEPA
Image captionBwana Madurio ameweka jeshi katika hali ya tahadhari
Hakuna majeraha yaliyoripotiwa.
Bwana Madurio ameweka jeshi katika hali ya tahadhari
Polisi huyo alijitambua kama Oscar Perez kupitia video iliyochapishwa kwenyr mtandao wa Instagram.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment