Boko Haram washambulia tena Nigeria


Wapiganaji wa Boko HaramHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWapiganaji wa Boko Haram
Wapiganaji wa Boko Haram wamefanya mashambilizi makali katika mji ulioko kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Watu walioshuhudia wanasema mashambulizi hayo makali yametokea wakati waislamu wakijiandaa kufuturu katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Picha ya video ambayo haijathibitishwa iliyotumwa katika mtandao wa Twitter inaonesha wanawake na watoto wakikimbia kutokana na mashambulizi hayo.
Gavana wa mji huo Kashim Shettima ameiambia BBC kwamba kulikuwa na majeruhi.
Lakini hata hivyo amesema jeshi la nchi hiyo limejibu mashambulizi na mji tayari ni shwari.
Wapiganaji wa Boko Haram wameteketeza eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria kwa kuua maelfu ya watu na kulazimisha wengine milioni mbili kuyakimbia makaazi yao.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment