WAKAZI 122 MKOANI SIMIYU WAPEWA HATI NA WAZIRI LUKUVI AGAWA HATI 122 LAMADI


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi amegawa hati miliki za ardhi 122 kwa wananchi wa Lamadi Mkoa wa Simiyu wakati alipofanya ziara yake mikoa ya kanda ya ziwa kuhamasisha ulipaji kodi ya pango la ardhi na suala la urasimishaji wa makazi holela.

Wananchi hao 122 ni wale waliofanikiwa kulipia michango yote, hivyo kuondokana na makazi holela na kuishi katika makazi rasmi. Hata hivyo jumla ya wananchi 5,200 wa Lamadi Mkoa wa Simiyu washapimiwa maeneo yao kwa ajili ya urasimishaji, na watapatiwa hati zao mara tu baada ya kukamilisha michango stahili.

Katika ziara hiyo, waziri Lukuvi amefika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza na kufanya ukaguzi wa mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi wilayani hapo na kugundua kati ya wakazi 35,000 wanaotakiwa kulipa kodi ya ardhi 28,000 wameishapelekewa hati ya madai.

Waziri Lukuvi pia ametembelea Idara ya Ardhi ya wilayani Nyamagana na kukagua mafaili ya kumbukumbu za wananchi kuhusu taarifa za ardhi ikiwemo masuala ya hati na kukugundua baadhi ya viongozi hawajalipa kodi ya pango la ardhi. Mmoja ya viongozi hao ni Mbunge wa Kwimba Shannif Mansoor ambaye hajalipa kodi ya pango la ardhi tangu 2010 kiasi cha shilingi milioni 529.

Aidha katika wilaya hiyo ameongea na wananchi wa Nundu kata ya Meko, mbali ya kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi papo hapo, amewahimiza kuchamkia fursa ya kurasimisha makazi yao na kupata hati ili kuzipa thamani ardhi zao na kujitanulia fursa za uchumi.
Magere Mugeta mkazi wa Lamadi mkoani Simiyu akipokea hati ya kumuliki ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi.
Janet Magige mkazi wa Lamadi mkoani Simiyu akipokea hati ya kumuliki ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akiwasisitiza wakazi Lamadi mkoani Simiyu umuhimu wa kumiliki ardhi kwa hati kwa kuwaonesha moja ya hati zinazotolewa kwa wananchi.
Wakazi wa Lamadi mkoani Simiyu wakishangilia pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi kwa kuwawezesha kupata Hati za kumiliki Ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akikagua moja ya faili katika masijala ya Ardhi ya Ilemela Mkoani Mwanza akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela (mwenye kofia).
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akikagua mfumo wa kodi wa manispaa ya Nyamagana mkoani Mwanza ili kubaini wadaiwa wa kodi ya Ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akiongea na wakazi wa Ilemela mkoani Mwanza.
Baadhi ya wakazi wa Ilemela mkoani Mwanza wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi alipokuja kusikiliza kero zao za ardhi.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment