TSN GROUP SASA YAJIKITA ZAIDI KATIKA KUSAIDIA JAMII KATIKA MAENEO YA VIJIJINI YENYA MAHITAJI MAALUMU NI KUPITIA TSN FOUNDATION...TAZAMA PICHA NA TUKIO ZIMA HUKO MUHEZA TANGA..


Msaidizi Binafsi wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa TSN Group inayomiliki makampuni mengine ya TSN Oil,TSN Logistics,TSN Supermarkets na TSN Distribution ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha mahusiano ya umma Ndg. Allan Halid Kiluvia akishiriki maandamano ya kuadhimisha siku ya wauguzi duniani ambayo yalifanyika wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga tarehe 11.05.2017.

Maashimisho haya yalienda sambamba na harambee ya kutunisha mfuko wa umoja wa wauguzi wilaya ya Muheza ambapo zaidi ya shilingi milioni nane za kitanzania zilikusanywa kama sehemu ya ahadi na pesa taslimu.

TSN Group ilitoa zaidi ya shilingi milioni moja za kitanzania huku lengo likiwa ni kukusanya shilingi milioni saba za kitanzania.

TSN Group imeahidi kupeleka maendeleo kwa kasi katika wilaya ya Muheza na sehemu zingine nchini kwa kushirikiana na serikali huku ikiahidi kufufua shughuli za TSN Foundation katika kutekeleza ahadi hizo.


Katika harambee hii mgeni rasmi alikuwa Ndg.Allan Halid Kiluvia aliyemwakilisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa TSN Group Ndg.Farough Ahmed Abood Baghoza.

SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment