Rais Buhari aonekana hadharani kwa mara ya kwanza.... Hii ni baada ya tetesi za mdamrefu kuwa alikuwa anaumwa na afya yake kuleta minong'ono kwa Wananchi wa taifa hilo..


Rais wa Nigeria, Mohammadu Buhari
Image captionRais wa Nigeria, Mohammadu Buhari
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya wiki moja.
Mkanda mfupi wa video, unamuonyesha Bw Buhari akizungumza na watu, baada ya kutoka msikitini kwa swala ya Ijumaa katika Ikulu ya Rais.
Maafisa wake wa mawasiliano pia wamepakia picha zake akitembea kutoka msikiti huo katika ikulu ya rais kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.
Rais Buhari akiwa msikitini IjumaaHaki miliki ya pichaTWITER
Image captionRais Buhari akiwa msikitini Ijumaa
Kumekuwepo na wasiwasi kuhusiana na afya ya Rais huyo, kwani hajaonekana hadharani tangu aliporejea Nigeria kutoka kwa ziara ya matibabu ya wiki saba nchini Uingereza, alipokwenda kutibiwa ugonjwa ambao bado haujajulikana.
Pia hajahudhuria mikutano mitatu ya baraza la mawaziri, na hakuhudhuria maombi ya ijumaa msikitini juma lililopita.
Lakini washauri wake wanasema kwamba, alikuwa akipumzika huku akifanya kazi akiwa nyumbani.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment