MWENYEKITI WA KIJIJI CHA IKUNGI ATUMBULIWA JIBU KWA VULIWA MDARAKA


Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ikungi waliohudhuria mkutano maalum wa kijijji hicho wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu hayupo pichani.Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu katikati akiwa na kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Haika Massawe na kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho Athuman Seleman wakiwa kwenye mkutano maalum wa kijiji.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akizungumza na wananchi hawapo pichani kwenye mkutano maalum wa kijiji cha ikungi,kulia kwake ni kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho Athuman Seleman na kushoto kwake ni kaimu mkurugenzi wa halmashauri Haika Massawe.
Mkaguzi wa ndani wa halmashauri ya Ikungi Kitundu Mkumbo akisoma taarifa ya ukaguzi mbele ya mkutano maalum wa kijiji cha Ikungi.

………………………………………………………………….

MKUTANO maalum wa Kijiji cha Ikungi wilayani Ikungi mkoani Singida umemuondoa Mwenyekiti wa kijiji hicho Hussein Ikusi kutokana na matumizi mabaya ya madaraka kwa kufanya ubadhirifu wa mali za kijiji zenye thamani ya shilingi milioni 9.

Ubadhirifu huo aliufanya toka alipoingia madarakani mwaka 2014 akishirikiana na aliyekuwa mtendaji wa kijiji hicho Hamis Isango aliyehamishiwa kijiji cha Irisya.

Hayo yalibainika baada ya halmashauri ya kijiji kuitisha kikao maalum tarehe 24 aprili mwaka 2017 wakimtuhumu mwenyekiti kwa hoja zipatazo 5.

Hoja hizo ni kushindwa kusimamia mali za kijiji,kushindwa kusimamia mipaka ya kijiji,kushindwa kuonyesha ushirikiano na uongozi wa halmashauri ya wilaya,Ofisi ya mkuu wa wilaya na taasisi za serikali zilizopo wilayani,kuwa chanzo cha migogoro badala ya kuwa mtatuzi na kushindwa kusimamia usomaji wa mapato na matumizi ya kijiji kwa mujibu wa sheria kwa kipindi cha miaka miwili na nusu.

Ubadhirifu huo umebainishwa na mkaguzi wa mahesabu ya ndani Kitundu Mkumbo aliyeagizwa na mkuu wa wilaya hiyo Miraji Mtaturu kufanya ukaguzi wa mapato na matumizi ya kijiji baada ya kupokea tuhuma kuhusiana na mwenyekiti huyo.

Akizungumza katika kikao cha kutoa taarifa kuhusiana na maamuzi yaliyoafikiwa na halmashauri ya kijiji Mtaturu alimuagiza kaimu mkurugenzi wa halmashauri Haika Massawe kumsimamisha kazi mtendaji wa kijiji cha Irisya Hamis Isango aliyehamishiwa kijiji kingine ili arudi ikungi kujibu tuhuma za kuondoka na vitabu 12 vya kukusanyia mapato alivyoshindwa kukabidhi wakati anahama ikiwemo na kutoa maelezo ya fedha zilizoonekana kupotea mikononi mwake.

“Bwana Ikusi kabidhi fedha na mali kama ushauri wa mkaguzi wa mahesabu alioutoa hapa mbele ya wananchi”alisisitiza Mtaturu.

Aprili 24 mwaka huu halmashauri ya kijiji iliazimia kwa kauli moja kumuondoa mwenyekiti huyo kutokana na tuhuma hizo dhidi yake huku huku ikisisitiza kuwa Usimamizi wa Rasilimali za Umma ni mabadiliko Chanya kwa maendeleo ya Ikungi.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment