MASIKINI KUMBE 'JAMBAZI' ALIYEUAWA JUZI KURASINI AKIDAIWA KUTAKA KUPORA MAMILIONI NI MWANAFUNZI WA UDSM....SOMAKWA.KIRWFU HAPA CHINIKUFUATIA MAUAJI YANAYOENDELEA NA HASA KUFUATIA MAUAJI YA KIJANA SALUM MOHAMED KURASINI HAPO JANA SHEIKH PONDA ISSA PONDA AMEMWANDIKIA MHE WAZIRI WA MAMBO YA NDANI UJUMBE UFUATAO NA KUHITAJI KAULI YA SERIKALI JUU YA MAUAJI HAYA. 

Mheshimiwa Waziri Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani, nakusalimu sana. Pia nakutakia ufanisi katika kulitumikia Taifa. Baada ya hayo ninayo haya ya kusema. Katika baadhi ya hafla nilizohutubia hivi karibuni, nilitumia fursa hiyo kueleza masikitiko yangu kwa mauwaji ya askari Polisi zaidi ya watano waliouliwa na watu wasiojulikana hivi karibuni Mkoani Pwani.

Natumia fursea hii pia kwako kutamka hivyo. 

Aidha jana tarehe 14 Mei, 2017, nilipokea taarifa ya kijana Salum Muhamed Almasi aliyeuwawa hadharani kwa kupigwa risasi na Polisi majira ya saa 3:00, na saa 4:00, asubuhi eneo la Kurasini Dar es Salaam akiwa anatembea barabarani kwa miguu. 

Taarifa ya Polisi ni kuwa kijana huyo ni jambzi aliyetaka kupora fedha.

Nimekutana na familia ya Marehemu ambaye ni mzaliwa wa Kilwa, familia inamtambua kuwa ni kijana mwema kabisa. Nimeongea na baadhi ya wakazi wa Kilwa, wao pia wanamtambua kama mtu mwema kwa tabia na anayeshiriki ibada Msikitini ipasavyo. 

Salum Mohamedi pia ni Imamu Msaidizi katika moja ya Misikiti Kurasini. 

Maelezo ya ziada Salum muda mwingi ni mtu wa masomo. Amemaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne, cha Tano, Kidato cha Sita na mpaka anauwawa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ngazi ya Diploma fani ya ICT Network. 

Mh. Waziri mauwaji kama haya yanazidi kupambamoto Tanzania na yanachafua haiba ya Taifa. Gazeti la Mwananchi la Mei 6, 2017, lilikuwa na kichwa cha habari kisemacho "WALIOUWAWA RUFIJI WAFIKIA 29".

Jambo la kuzingatiwa ni kwamba kwa utaratibu huu unaoshamiri, Wananchi wanaouliwa ndugu zao au jamii kwa ujumla wanapoteza haki ya kujuwa ndugu au raia wenzao ni wahalifu kweli au wanauwawa kwa sababu nyingine?

Utaratibu wa nchi hii uliowekwa, ni mtu kuadhibiwa kwa kufungwa, kutozwa faini, kuachiwa huru au kuuwawa baada ya kuthibitika kosa na kuhukumiwa.

Utaratibu huo ni wa kitaalamu 
/kisheria na ndio unaotumika katika Serikali zote bora duniani. 

Sisi tumeshuhudia ulivyo tufikisha katika Taifa (Tanzania), lenye utulivu na mahusiano mazuri kwa kiasi fulani kati ya Jamii na vyombo vya Dola. Vilevile umetufikisha katika Taifa la kistaarabu lisilofurahishwa na umwagaji wa damu kiholela. 

Ni vizuri Serikali ikatowa tamko la kufafanuwa sababu inayopelekea watu wengi kiasi hicho kuuwawa bila ya kufikishwa Mahakamani.

Ni malizie kwakusema, ikiwa mfumo wa nchi tuliourithi wa Mahakama, Bunge na Serikali una upungufu, basi busara ni kuuboresha na sio kuuhama na kuanzisha utaratibu mwingine kinyemela.

Natanguliza shukrani nikiwa na matumaini kuwa haya niliyoyazungumza yatazingatiwa.

Ahsante 

Sheikh Ponda Issa Ponda.SHARE

 • Image
 • Image
 • Image
 • Image
 • Image
  Blogger Comment
  Facebook Comment

1 comments:

 1. Nyerere aliwahi kunena haya"Ukianza kula nyama ya mtu, hutaacha utazoe" Leo taifa letu limefikia hatu ya kuto kuthaminiana na kuheshimiana, taifa la kuona damu ya mtu ni jambo la kawaida, nasema hivyo kwa sababu, Jeshi letu polisi limefikia hatua ya kumwaga damu za watanzania kwa kigezo cha uhalifu. (ujambazi). Sheria za nchi zipo wazi kama una mshuku mtu kutokana na mwenendo wake, mkamate mfikishe kwenye nyombo vya kisheria ashuhulikiwe, na sio kukatisha uhai wake. Madhara yake ni makubwa, kwani huacha majeraha kwa famili na kujenga chuki dhidi ya serekali yao. Hizi ni damu za watanzania wasio na hatia. Haingii alikini kuwa raia mpita njia akapigwa risasi kwa madai ya ujambazi ili hali hana hata jiwe mkononi. Tahadharini jeshi letu la Polisi, wenzetu Rwanda mwaka 94, yaliyotokea tunafahamu.Askari wengi ni vijana wa miaka 95, Yaliotoke Rwanda kwao ni kama historia. Ila kwa tulioshuhudia,tuna waomba hii ni nchi yetu sote tuliorithi kutoka kwa mababu zetu nasi tutawaachia wajukuu zetu. Mungu ibariki Tanzania

  ReplyDelete