LG YAZINDUA BIDHAA YA MPYA YA KIYOYOZI INAYOTUMIA UMEME MDOGO NA RAFIKI KWA MAZINGIRA


KAMPUNI ya vifaa vya Umeme ya Life is Good (LG) imezindua  viyoyozi  ambavyo ni rafiki kwa mazingira kwa gharama za kuweza kumuda kwa kila mtanzania.
Akizungumza na katika  hafla ya uzinduzi wa viyoyozi  hivyo , Kaimu Mkurugenzi wa Idara Ushauri wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA), Mhandisi Mtapuli Juma amesema vifaa vya LG vina ubora katika matumizi ya nishati ya umeme.
Amesema kuwa  kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ni muhimu  kutumia vifaa vya umeme ambavyo ni rafiki wa mazingira bila kufanya hivyo  itakuwa tunaharibu mazingira kwa vizazi vijavyo.
Amesema kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hakuna mtu anayeweza kukwepa katika kutumia vifaa ambavyo vinakuwa ni rafiki wa mazingira.
Nae Mkurugenzi Mtendaji LG Electronics Afrika Logistics, Janghoon Chung,  amesema kuwa wamefanya utafiti na kuona kuna mahitaji ya viyoyozi ambavyo vitakuwa ni rafiki wa mazingira na kutaka  watu watumie bidhaa hiyo.
Amesema viyoyozi hivyo vinatumia nishati ndogo hali ambayo inafanya kila mtu kuweza kumudu matumizi ya viyoyozi pamoja na kulinda mazingira.
Aidha amesema kuwa watu wanatakiwa kutumia vifaa ambavyo vinakuwa rafiki wa mazingira ambapo LG wameweza kuzalisha bidhaa kutokana na mahitaji ya sasa yaliyopo.

 Kaimu Mkurugenzi wa Idara Ushauri wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA), Mhandisi Mtapuli Juma akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa viyoyozi iliyofanyika leo  katika Hoteli ya Hyatt Legency jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji LG Electronics Afrika Logistics, Janghoon Chung akingumza na waandishi habari juu ya ubora wa viyoyozi vya LG iliyofanyika leo  katika Hoteli ya Hyatt Legency jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Masoko Afrika Mashariki LG Electronics , Moses Marji  akizungumza wakati wa  uzinduzi wa bidhaa mpya kutoka LG 
Meneja wa bidhaa za LG Afrika Mhandisi , Singh Chana  akizungumza juu ya umuhimu wa bidhaa za LG katika uhifadhi wa Mazingira .
 Mkurugenzi Mtendaji LG Electronics Afrika Logistics, Janghoon Chung Akimkabidhi zawadi ya Televisheni mmoja wa washindi wa bahati nasibu  iliyochezeshwa katika semina ya uzinduzi wa bidhaa mpya za Lg Tanzania , Ramachandran  Veeraman
 Watumbuizaji wa bendi ya Borabora wakiwa wanatoa burudani jukwaani
Bendi ya muziki ya Borabora ikitoa burudani kwa watu waliofika katika mkutano huo
sehemu ya wafanyakazi wa LG wakiwa katika picha ya pamoja
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment