Kiongozi wa zamani wa FBI kuchunguza iwapo Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani


Robert Mueller aliingoza FBI kuanzia 2001 - 2013
Image captionRobert Mueller aliingoza FBI kuanzia 2001 - 2013
Wizara ya sheria nchini Marekani, imetangaza kuteuliwa kwa mwendesha mashtaka maalum atakae ongoza uchuguzi wa tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa marekani wa mwaka jana.
Mwendesha mashtaka huyo aliwahi kuwa mkuu wa shirika la kijajusi la FBI, Robert Mueller.
Pia katika uchunguzi wake, atazingatia iwapo kulikuwa na mwingiliano wa aina yoyote kati ya Urusi na timu ya kampeni ya Trump.
Taarifa iliyotolewa na wizara ya sheria nchini humo imesema uchunguzi huo utaongozwa na mtu asiyeegemea upande wowote kwa ajili ya maslahi ya umma.
Tangazo hilo linafuatia utata uliogubikwa kufuatia kufutwa kazi kwa wiki moja iliyopita kwa James Comey, ambae ndie aliyekuwa akiongoza uchunguzi huo.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment