JUKWAA LA HAKI NA USALAMA LAZINDUA NA KUGAWA TOLEO MAALUMU LA NUKTA NUNDULA KITABU MAALUM CHAPISHO JUU YA MAMBO 101 KUHUSU POLISI..

 Ofisa Elimu Maalum Wilaya Ilala, Salehe Msechu wa pili kutoka kulia akionesha kitabu cha nukta nundu, katika hafla ya kukabidhi vitabu 20 vya nukta nundu  kwa ajili ya wanafunzi wasioona katika Shule ya Uhuru Mchanganyiko jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Madeline Kimei, akifuatiwa na Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wasiona Tanzania, Jonas Lubago na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana. (PICHA NA SULEIMAN MSUYA)  

JUKWAA la Haki na Usalama linatarajia kugawa vitabu 7,000 ambavyo vimebeba ujumbe kuhusu mambo 101 mwananchi anapaswa kuyajua kuhusu polisi huku vitabu 300 vikilenga watu wenye mahitaji maalum. Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Madeline Kimei wakati akizindua na kukabidhi vitabu 20 vya nukta nundu kwa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam leo. 


SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment