Polisi Ujerumani: shambulizi la Dortmund halikuwa la kigaidi


Gari la Dortmund lililengwa na milipuko mitatu
Image captionGari la Dortmund lililengwa na milipuko mitatu

Polisi Ujerumani: shambulizi la Dortmund halikuwa la kigaidi

Polisi nchini Ujerumani imesema kuwa gari lililokuwa limewabeba wachezaji wa Borussia Dortmund kuelekea katika mchezo wa nyumbani kwenye ligi ya mabingwa Ulaya lililengwa na milipuko mitatu.
Katika mkutano na waandishi wa habari, wamesema kuwa barua ilikutwa pembezoni mwa eneo la shambulizi hilo,lakini haikuwa na maelezo ya kutosha.
Polisi imekana kuwa ni shambulizi la kigaidi.
Mchezaji mmoja wa Dortmund na raia wa Uhispania Marc Bartra amejeruhiwa na kufanyiwa upasuaji.
Mlinzi Marc Bartra amejeruhiwa katika shambulizi hilo
Image captionMlinzi Marc Bartra amejeruhiwa katika shambulizi hilo
Taarifa za kiintelijensia zinasema kuwa zinachunguza shambulizi hilo kama linahusika na mashabiki wa timu ya upinzani.
Mchezo kati ya Dortmund na Monaco umeahirishwa mpaka Jumatano.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment