MKUU WA WILAYA MKURANGA AFUNGUA MAFUNZO YA KILIMO BORAMkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filbeto Sanga akizungumza na wakulima,wapuliziaji dawa wa korosho wa mkoa wa Pwani katika mafunzo ya kilimo bora na matumizi sahihi ya viuatilifu, leo mkoani Pwani
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde akizungumza na wakulima,wapuliziaji dawa wa korosho wa mkoa wa Pwani.
Mwakilishi wa Mkurugenzi kanda ya kusini ARI-NALIENDELE Dr Shamte Shomari akizungumza na wakulima,wapuliziaji dawa wa korosho wa mkoa wa Pwani.

 wakulima,wapuliziaji dawa wa korosho wa mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filbeto Sanga.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filbeto Sanga akiwa katika picha ya pamoja na wakulima,wapuliziaji dawa wa korosho wa mkoa wa Pwani.picha zote na Emmanuel Massa,Globu ya Jamii.
SERIKALI kupitia Bodi ya Korosho Tanzania imejipanga kuhakikisha pembejeo za korosho kwa`msimu ujao wa`mwaka 2017/18 kwa wakulima wa zao la korosho zinawafikia wakuima kwa`wakati kwani mpaka sasa tani 2,890 za Salfa ya unga na lita 30,000 za viatilifu vya maji zimeshawasili katika Bandari ya Dar es Slalaam.

Akifungua mafunzo ya kilimo bora na matumizi sahihi ya viuatilifu kwa wakulima na wapuliziaji dawa wa Mkoa wa Pwani,Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbeto Sanga amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa nafasi ya kuwafunza wawakilishi wa wakulima na wadau wa zao la korosho namna ya kuhudumia zao hilo.

Alisema katika msimu uliopita wa mwaka 2016/17 upatikanaji na usambazaji wa pembejeo za ruzuku za zao la korosho ulikuwa wa kuridhisha kutokana na kupatikana kwa fedha za ushuru wa mauzo ya korosho nje ya nchi kwa wakati kulikowezesha uagizaji wa pembejeo nao ufanyike kwa wakati.

“Kupatikana kwa fedha za ushuru wa mauzo ya korosho nje ya nchi kwa wakati kuliwezesha uagizaji wa pembejeo ufanyike kwa wakati hivyo kumfikia mkulima kabla ya muda wa kupuliza dawa kwenye mikorosho haujafika,”amesema Sanga.

Aliongeza kuwa, kiasi cha pembejeo kilichoagizwa kilikuwa cha kuridhisha mpaka sasa bado vipo viuatilifu vilivyobaki katika maghala ya Mwendapole Kibaha na Naliendele Mtwara pamoja na Mtwara mjini.

Alisema katika msimu wa`mwaka 2017/18 serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania inejipanga vizuri kuhakikisha kuwa pembejeo za korosho zinawafikia wakulima kwa wakati kwani mpaka sasa tani 2,890 za salfa yaunga na lita 30,000 za viuatilifu vya maji zimeishawasili katika bandari ya Dar es Salaam na ziko katika hatua ya kusafirishwa katika vituo vilivyotengwa katika Halmashauri zote.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania ambaye ni Mwenyekiti tawi la Dar es Salaam Mangile Malegesi ambao ndiyo waandaaji wa mafunzo hayo amesema mbegu zilizowasili zinatarajiwa kuanza kutolewa mwezi ujao.

Hata hivyo alisema mafunzo haya yamelenga kuifikia mikoa inayojishughuisha na zao hilo ambayo ni mkoa wa Pwani,Tanga ambapo awamu ya pili itakuwa ni mikoa ya Mtwara, Lindi,na Ruvuma. 
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment