Marekani yapeleka meli za kivita katika rasi ya Korea


Meli ya Carl Vinson kwa sasa inaelekea rasi ya KoreaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMeli ya Carl Vinson kwa sasa inaelekea rasi ya Korea
Jeshi la Marekani limetoa amri kwa meli zake za kivita zinazobeba silaha zielekee karibu na rasi ya Korea, huku kukiwa na hofu kubwa kuhusiana na Korea Kaskazini kuimarisha silaha zake za kinukilia.
Msimamizi wa kijeshi wa Marekani wa eneo la Pacific alieleza kuwa kujiandaa huko kijeshi ni muhimu katika eneo hilo.
Meli hizo zinazojulikana kwa pamoja kama The Carl Vinson Strike Group zinashirikisha meli moja kubwa ya kubeba ndege za kivita na meli zingine za kivita za kawaida.
Meli ya Carl Vinson (katikati) ikisindikizwa na meli zingineHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMeli ya Carl Vinson (katikati) ikisindikizwa na meli zingine
Awali ndege hizo zilitarajiwa kuzuru Australia lakini mkondo wake ukabadiliwa kuelekea Bahari ya Pacific.
Eneo hilo la Pacific ni kule ambako wanajeshi wa Marekani walifanya mazoezi ya kijeshi na wanamaji wa Korea Kusini.
Msemaji wa jeshi la Marekani anasema kuwa Korea Kaskazini ndilo tisho kubwa zaidi kwa usalama wa eneo la Pacific.
Meli ya Carl Vinson hubeba ndege aina ya F/A-18F Super HornetsHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMeli ya Carl Vinson hubeba ndege aina ya F/A-18F Super Hornets
Anasema ushahidi ni jinsi taifa hilo linavyofanya mazoezi ya zana za kinukilia kiholela.
Mbali na kuwa na uwezo mkubwa wa kushambulia, meli hizo za kivita zina makombora yanayoweza kuzima zana zo zote zinazolengwa kwake.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment