Mali ya Ivanka Trump na mumewe yafichuliwa


Mali ya Ivanka Trump na mumewe yafichuliwaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMali ya Ivanka Trump na mumewe yafichuliwa
Ikulu ya Marekani, imetoa maelezo kuhusu mali ya binafsi ya watu waliomo katika serikali ya Rais Donald Trump.
Mali hiyo imedhihirishwa kama sheria inavyoelekeza, na inaonyesha kuwa mtoto wa rais wa kike, Ivanka pamoja na mumewe Jared Kushner, wana takriban dola milioni 240 na 740 mtawalia.
Hii ni pamoja na hisa kwenye hoteli ya Trump International, ambazo zilimpa Ivanka kati ya dola milioni 1 na milioni 5 mwaka uliopita.
Ufichuzi huo wa mali pia unaonyesha mishahara na watu wengine wa vyeo vya juu uongozini.
Nyaraka zilizotolewa pia zilionyesha mali wakati wakianza kuifanyika kazi serikali na kabla la mali yoyote kuuzwa
Ikulu ya White House inajaribu kuonyesha kuwa watu katika serikali ya Trump wanajiweza, na inasema watu hao wamejitolea sana kwa kukubali kutumika serikalini.
Watu walio kwenye baraza la mawaziri la bwana Trump wana jumla ya mali ya dola bilioni 12.
Watu walio kwenye baraza la mawaziri la bwana Trump wana jumla ya mali ya dola bilioni 12.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWatu walio kwenye baraza la mawaziri la bwana Trump wana jumla ya mali ya dola bilioni 12.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment