China yazindua meli kubwa ya kubeba ndege za kivita


Vyombo vya habari vya serikali ya Chian vimesambaza picha za manowari hiyo ikiwa imerembeshwa kwa mapamboHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionVyombo vya habari vya serikali ya China vimesambaza picha za manowari hiyo ikiwa imerembeshwa kwa mapambo
China imetangaza kwamba imefanikiwa kuzindua manowari yake ya kwanza ya kujiundia yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita.
Meli hiyo ya kivita ina uzani wa tani 50,000.
Hatua hiyo inachukuliwa kama ishara ya karibuni zaidi ya kujiimarisha kwa taifa hilo katika nguvu za jeshi lake la majini.
Vyombo vya habari nchini China vinasema meli hiyo, ambayo inawezesha ndege kuruka na kutua juu yake, ilisafirishwa kutoka eneo ambalo ilikuwa ikiundiwa Dalian na kuwekwa baharini.
Inatarajiwa kuanza kazi rasmi mwaka 2020.
Kulinganisha meli kubwa za kivita za kubeba ndege
Image captionKulinganisha meli kubwa za kivita za kubeba ndege
Meli hiyo ya kivita ilizinduliwa DalianHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMeli hiyo ya kivita ilizinduliwa Dalian
Meli hiyo baada ya kung'oa nanga DalianHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMeli hiyo baada ya kung'oa nanga Dalian
Meli pekee kubwa ya kubeba ndege inayomilikiwa na China ni meli ya Liaonong, ambayo ni meli ya enzi za muungano wa Usovieti iliyofanyiwa ukarabati.
China ilinunua meli hiyo kutoka kwa Ukraine.
Liaoning Dalian, 22 Sept 2012Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMeli ya kwanza ya kubeba ndege ya China kwa Liaoning ilinunuliwa kutoka Ukraine
LiaoningHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMeli ya Liaoning ilipokuwa inakabidhiwa rasmi kwa jeshi la wanamaji la China Septemba 2012
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment