Almasi isio ya kawaida yaweka rekodi mpya katika mnada


Almasi ya waridi yavunja rekodi ya mauzo katika mnadaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionAlmasi ya waridi yavunja rekodi ya mauzo katika mnada
Almasi isio ya kawaida inayojulikana kama 'Pink Star' imeuzwa mjini Hong Kong kwa zaidi ya dola milioni 71 hivyobasi kuweka rekodi mpya kwa madini yoyote katika mnada.
Almsi hiyo yenye umbo la mviringo ilio na uzito wa karati 59.6 ilinunuliwa baada ya dakika tano katika eneo la Sotheby kulingana na ripoti.
Ndio almasi kubwa iliosafishwa katika kiwango chake kuwahi kupigwa mnada.
Iliuzwa kwa dola milioni 83 mjini Geneva 2013 lakini baadaye mnunuzi akashindwa.
Rekodi iliokuwepo ilishikiliwa na Oppenheimer Blue, ambayo iliuzwa kwa dola milioni 50 mnamo mwezi Mei.
Wakipiga mnada almasi hiyo iliopatikana na De Beers katika mgodi mmoja barani Afrika 1999, walianza kwa kuiuza kwa dola milioni 56.
Sotheby imesema kuwa mnunuzi wake ni muuzaji wa vito wa Hong Kong Chow Tai Fook.
Alexander Breckner, mkuu wa almasi katika duka la vito la Diamond 77 alisema kuwa jiwe hilo sio la kawaida.
''Ndio almasi kubwa ya rangi ya waridi kupatikana katika historia ya mwanadamu''.
''In rangi nzuri sana.Na ukubwa na uzuri wake tayari unaifanya kuwa almasi ya kipekee''.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment